Baby Lyrics by RAYVANNY


Mwanzo nilijua upo msalani
Kama sio uko utakuwa nyumba ya jirani
Nikapiga simu yako haipatikani
Ndio unapokea sa' hivi mummy
Upo sehemu gani

Hata kama sijajibu naomba Samahani
Ile njaa ya tumboni imepanda mpaka kichwani
Sijakuaga ila jua ndio nipo njiani
Ningependa niwe na wewe, ila uko utumwani
Ningependa niwe na wewe, ila uko utumwani

Inamaana umechoka sa mbona ni mapema
Hizo shida zimechosha ntazeeka mapema

Ni kweli ndani kuna masufuria
Chakula hakuna, nini nitakupikia
Na Kama tukipika basi bamia
Kutwa nzima na njaa kama ngamia

Nguzo ya upendo kusubiria
Kwa nini unashindwa nivumilia
Na mimi mbona ninakupigania
Mummy rudi nyumbani, Mola atajalia

Aaah siwezi, kwa nini?
Sirudi, sababu gani?
Siwezi, aaah
Sirudi

Nguo zangu zilivyochoka kama tambala ya deki
Zimetoboka unaweza kusema net
Huishi madeni, dukani kwa mangi mpaka bank
Na ukirudi nyumbani, mfukoni huna cent

Anapanga mola, kupata kukosa ridhiki
Akinipa nashukuru na kama nikikosa sibishi
Kwenye swala la mapenzi, mali si kitu iyoo
Kwenye mapenzi, moyo kioa kitu iyoo

Inamaana umechoka sa mbona ni mapema
Hizo shida zimechosha ntazeeka mapema

Ni kweli ndani kuna masufuria
Chakula hakuna, nini nitakupikia
Na Kama tukipika basi bamia
Kutwa nzima na njaa kama ngamia

Nguzo ya upendo kusubiria
Kwa nini unashindwa nivumilia
Na mimi mbona ninakupigania
Mummy rudi nyumbani, Mola atajalia

Aaah siwezi, kwa nini?
Sirudi, sababu gani?
Siwezi, aaah
Sirudi

Watch Video

About Baby

Album : Sound from Africa (Album)
Release Year : 2021
Copyright : (c) 2021 WCB Wasafi.
Added By : Huntyr Kelx
Published : Jan 30 , 2021

More lyrics from Sound from Africa album

More RAYVANNY Lyrics

RAYVANNY
RAYVANNY
RAYVANNY
RAYVANNY

Comments ( 1 )

.
okong mathias 2021-11-14 07:53:56

i never thought vanny would ever sing in english,buh diz z great coz it helps create more fans world wide



About AfrikaLyrics

Afrika Lyrics is the most diverse collection of African song lyrics and translations. Afrika Lyrics provides music lyrics from over 30 African countries and lyrics translations from over 10 African Languages into English and French

Follow Afrika Lyrics

© 2024, We Tell Africa Group Sarl