Lissa II Lyrics
Lissa II Lyrics by RAPCHA
Eugene sogea karibu kidogo
Kabla sijakata pumzi ya mwisho tuongee japo kidogo
Enjoy kila siku iyendayo kwa MUNGU
Kwenye maisha ya mwanadamu siku za furaha huwa ni ndogo
Sijapanga kumkufuru Muumba
Ila kwa leo ningemwomba arudishe tu masaa nyuma
Haya mateso nnayopata kwenye hiki kitanda
Damu yangu itamlilia Lissa haitokaa kimya
Mwambie asichelewe nitamsubiri Paradiso
Kama nitapona basi sitomsahau mpaka kifo
Kumbukumbu zitamfata kila unyayo
Amekatisha ndoto yangu kubwa niliyo nayo
Najua kabla hawajatangaza Lissa
Millard Ayo, Sam Misago, Simulizi watauliza kisa
We waambie nilikuwa nije niwe namba moja
Ila mtu mmoja tu ndoto yangu ameikatisha
Mwambie Mama sikuacha sala
Ugumu wa pesa ndo umefanya nishindwe kuja home kila mara
Pesa inatesa vibaya na ukiiweka mbele kabla ya MUNGU
Ndo mwanzo wa ubaya
Hii habari itamuumiza Majani
Plan zetu zote kubwa zimeishia njiani
Lile gari aliloniagizia ampe Mama
Please Kusah atamfundisha ku-Drive
Ataenda nalo Kanisani mhhh!
Mwambie father atalipwa na Mola
Arudishe moyo nyuma amsamehe Paula
Mwambie anitimizie ndoto kuni-sign Bongo Records
Wengi walikataa yeye akaona nyota inayong'ara
Mziki umeni-introduce kwenye maisha ambayo ngumu sana
Kumpata mpenzi aliye sahihi
Katika kuendelea kumtafuta ndo nkajikuta
Anaongeza list wanachuo mpaka wasanii
Kwangu alikosa kipi?
Akaamua aache seat kubwa niliyompa
Kwenye moyo akadandia lifti
Nilitulia ingawa wanawake
Wanaamini kuwa mwanaume hata
Akikupenda vipi lazima atakucheat
Nitakuwa mgeni wa nani mara ngapi Jumapili
Nilitii wito wako nkaacha kwenda Kanisani
Leo nakufa kitandani vilivyofanya mpaka
Nikawa mbali na MUNGU wangu sivioni
Kupeana mapresha tu, kwenye mapenzi
Watu hawaumizi expectations do
Wengine walitamba haikupita hata mwezi tu
Sasa hivi wako busy wanafuta tattoo
Kama ikitokea nikapona sitofanya revenge
Awe na amani maana amechagua maisha ya ku-trend
Wala msimchukie
Maana kila mtu ana mabaya yake
Tuna act tuko perfect tuna pretend
Unahisi ngoma zitaendelea kupigwa redioni
Nilitamani nipate tuzo zaidi ya pesa ya nguo
Mama angu Jidee ataumizwa sana na hii habari
Mwambie ahsante kwa kunshika mkono hii safari
Utaniagia mashabiki
Waliozimia ngoma zangu ndani na nje ya nchi
Inawezekana mziki bila kiki
Ila kiki ni kama madawa ukiyatumia hauachi
Wanangu nawatakia maisha marefu
Ka tutaonana badae tutaongea kwa kirefu
Wakumbushe Byser na Chatta watafute tu cash
'Cause you stop living when stop believing in yourself
Asante kwa kunisikiliza
Naitwa Rapcha last king of 90's baby
Watch Video
About Lissa II
More lyrics from Wanangu 99 album
More RAPCHA Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
You May also Like
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2024, We Tell Africa Group Sarl