So Sad Lyrics
So Sad Lyrics by YOUNG KILLER
Ha! Naamka asubuhi yoh baby mama ananitazama
Jana usiku nilimwambia kuwa kuna pahala nimekwama
Nikaplease tuombe Mungu leo kukuche salama
Nikatafuta nilewe kabla jua halijazama
Huwaga nimeolewa ila kwa hili hajanibelieve
Kuwa nitapata like you wa jana tumelala kwa maumivu
Hatujaweza bado, till now ni miaka 15
Tuko mbali na bado haijatimia adimu
But watoto wanaenda shule ila home taabu
Elimu bure ila changamoto ni ya vitabu
Vya kujisomea hasa kiswahili na hesabu
Wife ni mgonjwa kitambo anaendelea na matibabu
Kitu inaniuma ni kulala njaa na watoto
Wakinitazama kwa huruma wanajua ni changamoto
Mpanagaji Mungu, hustle haziwezi kuwa till I die
Bado siamini ng'ombe wa maskini hazai
So lemme try, tell me
Life is so sad
Life is so sad
Kuna muda uko less nakosa hata mood ya mapenzi
Put God first and watch your life changing
Believe in yourself is the secret to success
But dreams mingi zinakufaga kwa stress
Dear God we nifungulie milango
One kero za jirani anavyonishikia mabango
Zidi kunipoteza, ningewaweza ningewaharibia kitambo
Na kiukweli sina hata fedha na sijali hata pango
Please nionyeshe japo njia niweze pita
Sijapokea hata mshahara toka kwa boss mwezi wa sita
Simu zangu hashiki pia akiniona anakunja ndita
Na nyumbani hapakaliki hapa kana kwamba ni vita
Kitu inanichosha nikuwaza kesho kuna nini?
Najua nguvu ndo mtaji wa masikini na ninazo
Changamoto zisituletee vikwazo
I believe mwisho wetu huwezi kuwa kama mwanzo
Trust me beiby
Life is so sad
Take me away..
Napokea simu ya home kwamba wife kazidiwa
Kajaribu kuomba msaada kwa jirani kapatiwa
Ilionekana kuna kitu kinamtesa kwenye ziwa
Sijui ni presha au ni kitu kwenye titi kafanyiwa
Kimbia! Ukichelewa inaweza kuja kuwa hatari
Maana hawezi kuongea sauti inatoka kwa mbali
Kaingizwa ICU tunamngoja daktari
Tumwambie pesa mpaka uje kama atakubali
Njoo hospitali!
Watch Video
About So Sad
More YOUNG KILLER Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
You May also Like
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2025, We Tell Africa Group Sarl