Nenda Salama MAGUFULI Lyrics
Nenda Salama MAGUFULI Lyrics by WHOZU
Tunabaki na picha maneno ya kimaza
Hivi kweli umeondoka baba
Au ukute naota labda eeh
Kweli umetuheshimisha
Juhudi matendo yako
Hivi kweli umeondoka baba
Au ukute naota labda eeh
Imekuwa ngumu kuamini
Tunayempenda hatutamwona
Tunayempenda hayuko nasi tena
Imekuwa mapema hivi kwanini
La mwisho baba hata ungesema
Namwomba Mungu ulale mahali pema
Na asiyejua umuhimu, umuhimu wako baba
Atasherehekea kwa uvivu, uvivu wa fikra zake
Umeondoka mwalimu ingawa kifo ni ibada
Hayazoeleki maumivu
Baba umeondoka, umeondoka umetuacha
We nenda salama
Baba umeondoka, umeondoka umetuacha
We nenda salama
Japo Doctor umesha speech kuhusu uchumi wa kati
Wapo waliokudhihaki
ulipopambana na wale wengi walioidhulumu haki
Zile ngumu nyakati haukuwa na wasiwasi
OMG I can't believe leo umekuwa hayati
Si ni vigumu kutadhmini ila haina walakini
Kumpoteza aliyejisacrife kisa masikini
Aliweka kando umimi akafanya mambo mengi kwa usawa
Bila hata kujali kabila wala dini
Kweli binadamu wa sasa muda wetu ni mchache baba
Muda wetu ni mchache labda
Ukipata ata wasaa wa mwisho tupe neno la uzalendo
Labda kichwani mwetu ingebaki --
Baba umeondoka, umeondoka umetuacha
We nenda salama
Baba umeondoka, umeondoka umetuacha
We nenda salama
Yo baba mambo mengi umefanya
Kutumbua viongozi walopita njia za panya
Umeondoka baba nchi umeiacha salama
Ulazwe mahali pema japo mapema sana
Watch Video
About Nenda Salama MAGUFULI
More WHOZU Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
You May also Like
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2025, We Tell Africa Group Sarl