Bora Peke Yangu Lyrics
Bora Peke Yangu Lyrics by MACVOICE
(Eyoo Trone)
Heshima na upole wako
Ndivo vikanivuta kwako oh oh
Tabia na mwenendo wako oh
Vikanifanya nikupende eh eh
Kumbe mapenzi ni nyakati yanachanganya
Yakipoteza ramani wewe
Kitabu cha upendo wa dhati umechanachana
Haupo kama zamani wewe
Ngoma ikivuma mwisho wake hupasuka
Yote ya nini tuje kushikiana chupa
Wewe ukipanda kila muda mi nashuka
Oh ooh oh, oh oh oh
Message za watu wako na simu zako
Naona ila namezea tu
Najua machafu yako mabaya yako
Yanachoma mi napotea tu
Kugombana mi siwezi
Nikwambie yote sababu ya mapenzi
Tena narudisha jezi nitulie
Ligi ya mapenzi siwezi
Kwako wewe, bora peke yangu
Nibaki peke yangu
Bora peke yangu
Niishi maisha yangu
Bora peke yangu
Nibaki peke yangu
Bora peke yangu
Niishi maisha yangu
Uliweka pamba masikioni
Husikii huoni ninavyoumia moyoni
Purukushani asubuhi jioni
Matusi mdomoni hata aibu huoni
Ukadanganya unaenda sokoni
Kumbe yuko mgongoni kitandani ukingoni
Una wapenzi wengine kinondoni
Hadi Kigamboni na Kariakor shimoni
Ah wee, kumbe ni mnyama uloficha makucha
Hata sura yako inakusuta
Nyama ndani ngano nnje kama sambusa
Barafu wa moyo umeyeyuka
(Oh wo wo wo wo, oh wo wo wo wo)
Hukunipenda, pengine nilikulazimisha
Sawa nakwenda, japo sina wa kuninyamazisha
Huna makosa najilaumu nini?
Nilikupenda kwa nini?
Ona kugombana mi siwezi
Nikwambie eti sababu ya mapenzi
Tena narudisha jezi nitulie
Ligi ya mapenzi siwezi
Kwako wewe, bora peke yangu
Nibaki peke yangu
Bora peke yangu
Niishi maisha yangu
Bora peke yangu
Nibaki peke yangu
Bora peke yangu
Niishi maisha yangu
(Nusder)
Watch Video
About Bora Peke Yangu
More lyrics from My Voice album
More MACVOICE Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
You May also Like
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2024, We Tell Africa Group Sarl