SARAH MAGESA Watasubiri cover image

Watasubiri Lyrics

Watasubiri Lyrics by SARAH MAGESA


Mimi sijafa bado naishi
Mimi sijafa bado naishi
Waliosubiri aibu yangu
Watasubiri sana
Watasubiri sana waliosubiri aibu yangu
Waliosubiri aibu yangu watasubiri sana
Mimi nipo sijafa
Nipo na Yesu wangu
Mimi sijafa bado naishi
Mimi sijafa bado naishi
Waliosubiri aibu yangu
Watasubiri sana
Nasema watasubiri sana
Watangoja sana
Waliosubiri aibu yangu
Watasubiri sana

Maadui wamenitegea mitego mingi
Lengo lao wanataka waniangamize
Maadui wamenitegea mitego mingi
Lengo lao wanataka wanimalize
Wananipa tabasamu la usoni
Kumbe moyo wao, unanipangia mabaya
Wananichekea tabasamu la usoni
Kumbe mioyo yao inampangia mabaya
Kupigwa vita ni kawaida hainisumbui
Mimi ni mti wenye matunda
Kupigwa vita ni kawaida hainisumbui
Mimi ni mti wenye matunda
Lazima nipigwe mawe
Lazima nipite kwenye moto

Mimi sijafa bado naishi
Mimi sijafa bado naishi
Waliosubiri aibu yangu
Watasubiri sana
Watasubiri sana
Waliosubiri aibu yangu
Waliosubiri aibu yangu
Watasubiri sana
Waliopanga nifukiwe
Ndio kwanza nainuliwa
Mimi sijafa bado naishi
Mimi sijafa bado naishi
Waliosubiri aibu yangu
Watasubiri sana
Matusi yao yameniweka viwango vingine
Waliosubiri aibu yangu
Watasubiri sana

Ninachojua walio upande wangu ni wengi
Kuliko walio upande wao
Ninachojua walio upande wangu ni wengi
Kuliko walio upande wao
Kile walichokipanga hakikufanikiwa
Maana mungu yupo upande wangu
Kile ulichonikusudia hakikufanikiwa
Maana mungu yupo pamoja na mimi
Nitalia kidogo nitanyamaza
Hata kama wameniumiza
Nitalia kidogo nitanyamaza
Ili nisiwafichulie wakaona wameniweza
Maana aliye ndani yangu ni mkuu sana
Kuliko aliye ndani yao
Kupigwa vita ni kawaida hainisumbui
Mimi ni mti wenye matunda
Kipigwa vita ni kawaida hainisumbui
Mimi ni mti wenye matunda
Lazima nipigwe nawe
Lazima nipite kwenye moto

Mimi sijafa bado naishi
Mimi sijafa bado naishi
Waliosubiri aibu yangu
Watasubiri sana
Bado nipo, nipo mimi sijafa
Waliosubiri aibu yangu
Watasubiri sana
Waliopanga nifukiwe
Ndio kwanza nainuliwa
Mimi sijafa bado naishi
Mimi sijafa bado naishi
Waliosubiri aibu yangu
Watasubiri sana
Matusi yao yameniweka viwango vingine
Waliosubiri aibu yangu
Watasubiri sana

Watch Video

About Watasubiri

Album : Watasubiri (Single)
Release Year : 2022
Copyright : ©2020 Administered By Msalaba MEDIA
Added By : Farida
Published : Aug 24 , 2022

More SARAH MAGESA Lyrics

SARAH MAGESA
SARAH MAGESA
SARAH MAGESA
SARAH MAGESA

Comments ( 0 )

No Comment yet



About AfrikaLyrics

Afrika Lyrics is the most diverse collection of African song lyrics and translations. Afrika Lyrics provides music lyrics from over 30 African countries and lyrics translations from over 10 African Languages into English and French

Follow Afrika Lyrics

© 2025, We Tell Africa Group Sarl