Fumbo Lyrics by KIBONGE WA YESU


Jana imepita
Leo ni siku mpya
Nimepata taarifa fulani ametutoka
Mbona nilikuwa naye jana, nashangaa
Mbona nilicheka naye sana, hapo nachoka eh
Mbona niliongea naye tena tukafurahi
Tukapanga mipango leo ameondoka eh
Kweli kifo ni fumbo
Ah ni fumbo
Mungu umetufumba, fumbo
Aah kweli kifo ni fumbo
Ah ni fumbo
Mungu umetufumba aah, fumbo

Usiringe , Duniani tunapita
Usiringe, Wewe ni maua
Usiringe , Duniani tunapita
Usiringe  Wewe ni maua
Wewe ni maua ua
Usiringe
Wewe ni maua ua
Usiringe
Wewe ni udongo udongoni utarudi
Usiringe
Sisi ni maua tunanyauka
Usiringe

Haya yote yanayotokea
Yanatukumbusha
Duniani sio kwetu, tunapita
Tena mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke eh
Siku zake si nyingi
Nazo zimejaa tabu sana
Kifo hakiangalii eti wewe ni mubabe, kinachukua
Kifo hakiangalii eti wewe ni mzuri sana
Tena hakiangalii wewe maarufu, kinachukua
Hakiangalii eti wewe ni mzuri sana, kinachukua tu
Maisha tumepewa ni dhamana
Kuwa hai tumepewa ni neema tu
Umepewa nafasi
Umepewa kipagi
Umepewa kibali
Vitumie vizuri
Kumbuka muda haulali
Yaja siku ya hatari
Ameificha maanani, wote hatuijui eeh

Usiringe duniani tunapita
Usiringe wewe  ni maua
Usiringe duniani tunapita
Usiringe wewe  ni maua
Wewe ni maua ua
Usiringe
Wewe ni maua ua
Usiringe
Wewe ni udongo udongoni utarudi
Usiringe
Sisi ni maua tunanyauka
Usiringe

Kifo ulimchukua mama yangu, fumbo
Ukamchukua baba yangu, fumbo
Kweli wewe ni fumbo, fumbo aah
Ukawachukua rafiki zangu, fumbo
Niliowapenda sana, fumbo
Wewe ni fumbo aaah
Fumbo, eeeeh
Kibo melodizer, naogopa fumbo

Watch Video

About Fumbo

Album : Fumbo (Single)
Release Year : 2022
Added By : Farida
Published : Jul 12 , 2022

More KIBONGE WA YESU Lyrics

KIBONGE WA YESU
KIBONGE WA YESU
KIBONGE WA YESU
KIBONGE WA YESU

Comments ( 0 )

No Comment yet



About AfrikaLyrics

Afrika Lyrics is the most diverse collection of African song lyrics and translations. Afrika Lyrics provides music lyrics from over 30 African countries and lyrics translations from over 10 African Languages into English and French

Follow Afrika Lyrics

© 2024, We Tell Africa Group Sarl