Ni Yule Yule Lyrics
Ni Yule Yule Lyrics by KIBONGE WA YESU
Haukuzaliwa kwa Bahati mbaya
haukuzaliwa uje uteseke
Haukuzaliwa kwa bahati mbaya
Haukuzaliwa maisha yakutese
Nakuona upo chini inakutesa mikopo
Umejawa na huzuni wakwe wanahitaji watoto
Nawe unalia lia una lia lia
Una lia na watesi wako
Wanauliza mbona hajibu
Huyo Mungu wako mbona hajibu
Eti nenda kwa waganga ukajaribu
Huenda nyota yako wameharibu
Wewe usihangaike kujibizana nao waambie
Ni Yule yule
Habadiliki habadiliki Mungu
Mungu Ni yule yule
Alie mpa sarah atanipa nami
Ni yule yule
Ooh Mungu ni yule yule Mungu
Mungu Ni Yule yule
Aliponya wakoma ataniponya nami
Ni yule yule
Alivusha wana israel nami nitavuta
Mungu Ni yule yule
Yee Mungu yee Mungu yee
Ni Yule yule
Awezae fanya mifupa ikaishi tena
Mungu ni yule yule
Ninajua wanatamka laana ili usifanikiwe
Ila Mungu atageuza baraka kwako na laana ziwarudie
Balam alipotaka kusema israel ulaaniwe
Akajikuta amesema ubarikiwe israel wewe
Goliath pamoja na dharau zake na kujigamba
Daudi mdogo akamuangusha
Usiogope ukubwa wa jaribu lako
Usiogope ukubwa wa tatizo lako wewe
Usiogope ukubwa wa watesi wako
Usiogope Mungu ni Yule yule
Wanauliza mbona hajibu
Huyo Mungu wako mbona hajibu
Eti nenda kwa waganga ukajaribu
Huenda nyota yako wameharibu
Wewe usihangaike kujibizana nao waambie
Ni Yule yule
Habadiliki habadiliki Mungu
Mungu Ni yule yule
Alie mpa sarah atanipa nami
Ni yule yule
Ooh Mungu ni yule yule Mungu
Mungu Ni Yule yule
Aliponya wakoma ataniponya nami
Ni yule yule
Alivusha wana israel nami nitavuta
Mungu Ni yule yule
Yee Mungu yee Mungu yee
Ni Yule yule
Awezae fanya mifupa ikaishi tena
Mungu ni yule yule
Kibo melodizer
Watch Video
About Ni Yule Yule
More KIBONGE WA YESU Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
You May also Like
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2024, We Tell Africa Group Sarl