NACHA My God cover image

My God Lyrics

My God Lyrics by NACHA


Mungu wangu, narudi kwako mi ni mwanao 
Ni mkosefu sijakamilika na sihitaji kuwa kama wao
Napiga goti nikiwa nimechoka
Nilikosea wapi nisahihishe upya?
Maana wenzangu wanapata mimi nakosa

Tazama nilivyo mnyonge na mwenye shauku kubwa ya kufanikiwa
Masikini mwenye ndoto nyingi za kusadikika zisizofanikiwa
Mungu wangu haujawai kushindwa 
Kama uliweza kufanya masika na kiangazi
Basi unaweza ukafanya na mimi pia nikapata kazi

Mungu wangu nivalishe nguo maana walimwengu wamenivua
Tena bila haya nayasema haya nikiwa 
Na akili timamu natambua jema na baya
Wamenitupa kwenye jua niungue, kwenye mvua nilowane
Nishushie mvuli wako wafadhaike Mungu wangu na watukane

Nifanye ning’are na nisihadaike nikavimba
Mi ni mende tu ila nifanye kila wakiniona wanione simba
Mungu, kama ulinileta duniani nikiwa nalia
Ni wazi ulitaka kunionesha dunia ni mbaya
Na walimwengu ni wabaya hawana haya ndio maana nayasema haya

Walishanitupia mawe na kunitishia uhai
Nikawaambie sihofii
Nikawaambie nina mungu wangu anayenilinda
Kwa hiyo wala sijutii
Nikawajibu namsikia Mungu tu
Nyinyi wasaliti vigeugeu wanadamu siwasikii
Wakanicheka sijapata nikawaambia hizo zote kudra
Mungu wangu ananipenda hanichukii
Na nikawajibu nitapata muda ukifika
Sababu mungu wangu hawahi wala hakawii

Mungu, duniani hakuna haki
Mwenye mabavu ni mabavu na mnyonge ni mnyonge
Hakuna usawa wala haki
Mungu wangu hujaziba masikio unanisikia
Huwa nageuza maneno yao machafu
Kuwa masafi na kisha nawarudishia
Labda mimi ni mshamba sana
Sijui kuvaa wenyewe wanaita fashion

Sipati michongo nimezubaa sana
Wenyewe huita connection
Natamani na mimi siku moja nipate
Nisahau kuhusu maumivu
Na nafanya kazi usiku na mchana
Sio kwamba mimi ni mvivu
Mi ni baba wa familia
Na niko na mke na watoto pia

Mi ndio muhimili nikilala njaa
Wamelala njaa na wao pia
Mungu tazama mi ndio baba mi ndio mama na hakuna kipato
Marafiki niliowaomba msaada
Waliishia kunijibu kila mtu atakula kwa jasho
Nyumbani dada yangu chausiku ni mgumba
Na anatamani mume na hajapata
Na wakati muda huo huo jirani alibarikiwa mtoto na anamtupa

Mungu wangu wainuwe wanawake wanaosalitiwa na kuonewa wanaume zao
Wanaoteseka na mapenzi wenye maumivu mazito kwenye mioyo yao
Na sio chombo cha starehe ni walinzi wa familia zetu
Na iko wazi pia mwanamke ni mungu wa pili na ni mama zetu
Kuna muda najiuliza au mi sistahili kuwa na maisha mazuri
Au sijui kuwa haubaki kumi kwenye mia ukitoa sufuri

Kwenye mafanikio marafiki ni wengi wazito na wepesi
Mungu wangu lakini kwenye shida
I see myself I see nobody nobody else dah!
Na kinachoniponza mi sio mbinafsi
Hata kipande kidogo cha mkate nataka tule wote
Lakini wao wakipata wanachotaka furaha yao ni mi nikose
Na mi ni mtu mmoja nimeamua kuweka wazi
Ila kuna wengi Mungu wangu
Wako chumbani wanajifungia wanalia kila siku
Wana maumivu na wanamwaga machozi

Mungu wangu kuna watu ni vipofu hawaoni
Wakati huo huo Mungu wangu wenzao wanaona
Na Wanaongezea mbwembwe za miwani machoni dah!
Sina msaada kwenye dimbwa hata nikipaza sauti
Nachoambulia ni kujibiwa kila nafsi itaonja umauti
Sihofii sumu zao nitawakanyaga vichwa
Hata kama wakiamua kufumba macho kila napopita
Ni kama sina bahati kila nikipanga Mungu haiwi
Nahitaji kusikia na unajua mi ni kiziwi
Najua mungu wangu una huruma

Mungu wangu unagawa kwa mafungu na upendeleo huna
Najiuliza ni wapi nilikwama nilikosea wapi
Au nilikuwa na radhi za mama sikukufuru 
Ah ah sina maana 
Ni kama nipo kwenye mlima mrefu pekee yangu nimesimama
Mungu umri unakwenda na matumaini yako wapi?

Hata nikijilazimisha furaha sipati
Najikaza nisiwe na tamaa ingawa nimechoshwa
Na maneno yana karaha
Nipe moyo wa subira nishinde haya majaribu
Moyo wangu una vidonda please Mungu vitibu
Natamani kuongea na mi ni bubu
Nimetengwa na marafiki mpaka na ndugu

Amani iko wapi? Duniani hakuko safi
Wengi wanakufa na stressi
Na ndoto zao kwenye nafsi
Ukingoja haki duniani unaumia

Ndio maana narudi kwako sio mbinafsi pumzi bure unanigawia
Ni kama nipo kwenye giza kinene hakuna taa wala mshumaa
Na muda wote nimesimama hakuna mahali pa kukaa
Miguu imechoka inatetemeka
Lakini nikikumbuka nilipotoka naongeza juhudi
Wakati wa Mungu ni kama maji kwenye bahari
Hakuna atakayeweza kuyadeki na haikwepeki

Hukunileta kwenye hii dunia kwa bahati mbaya
Ulikuwa una makusudi na sijachoka
Unajuwa mtaji wa masikini ni juhudi
Na ningeshakuwa nimewaza kutoa kafara
Tatizo sina akili za mgando
Hadi natamani niondoke kwenye hii dunia yao
Ya majungu fitina na masimango

(Nyasubi ndani ya mbanyu baby)

Watch Video

About My God

Album : My God (Album)
Release Year : 2020
Copyright : (c) 2020
Added By : Huntyr Kelx
Published : Mar 27 , 2020

More NACHA Lyrics

Comments ( 0 )

No Comment yet



About AfrikaLyrics

Afrika Lyrics is the most diverse collection of African song lyrics and translations. Afrika Lyrics provides music lyrics from over 30 African countries and lyrics translations from over 10 African Languages into English and French

Follow Afrika Lyrics

© 2025, We Tell Africa Group Sarl