
Nipo South Africa Lyrics
...
Nipo South Africa Lyrics by Msomali
Dully Kibody
Ahh Vitamin, yooh
Mwambie nipo South Africa
Nipo South Africaa
Aaahh
Unajua sikupenda kuondoka kuwa mbali na wewe
Mi mwenzako sikupenda kuondoka kukuacha mwenyewe
Mtunze sana huyo mwanangu
Itunze sana hiyo damu yangu
Nimemis kikongwe mama yangu
Nimewamiss wadogo wadogo zangu
Mwanangu akikuliza niko wapi
Mwambie nimekwenda mbali, nimekwenda kutafuta
Akikuliza tena, naomba mwambie
Nimekwenda mbali, nimekwenda kutafuta
Aking'ang'ania, naomba mwambie
Nimekwenda mbali, nimekwenda kutafuta
South Africa
Mwambie nipo South Africa
Nipo South Africa
Mwambie nipo South Africa
Mwambie nipo kiwanjani, kiwanjani
Asije leta tafarani, tafarani
Mwambie nipo kiwanjani, kiwanjani
Asije leta tafarani, tafarani
Tena umchunge, asije kuingia kwenye makundi mabaya
Naomba umchunge, asije kupewa jina la mtoto mbaya
Kusema nitarudi kesho, kesho kutwa
Ule msemo wangu umeuzoea
Mi nitarudi kesho, kesho kutwa
Ule msemo wangu umeuzoea
Mi labda nirudishwe kwenye sanduku nimekufa
Ila siyo kurudi kapuku nimechoka
Nirudishwe kwenye sanduku nimekufa
Ila siyo kurudi kapuku nimechoka
Mimi bora nirudishwe kwenye sanduku nimekufa
Ila siyo kurudi kapuku nimechoka
Nirudishwe kwenye sanduku nimekufa
Ila siyo kurudi kapuku nimechoka
Mwanangu akikuliza niko wapi
Mwambie nimekwenda mbali, nimekwenda kutafuta
Akikuliza tena, naomba mwambie
Nimekwenda mbali, nimekwenda kutafuta
Aking'ang'ania, naomba mwambie
Nimekwenda mbali, nimekwenda kutafuta
South Africa
Mwambie nipo South Africa
Nipo South Africa
Mwambie nipo South Africa
Juzi kati nimekoswa na bunduki South Africa
Nimekamatwa na kete, wamenishika
Mkono wa kulia hapa unapwita
Nimepigwa cha ukali yani, daaah
(Pole sana Baba mtu)
Dah, asante sana, asante sana Mama mtu
Respect watafutaji South Africa
Wapambanaji
Watch Video
About Nipo South Africa
More Msomali Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2025, We Tell Africa Group Sarl