FID Q Sumu cover image

Sumu Lyrics

Sumu Lyrics by FID Q


Aliyeniumba alinipa mdomo hivyo nina haki kuongea
Ni bahati nimeotea
Safi.. kamwe siachi kuishea
Hamtaki niwe fair
Trust me, mie huwa happy niki-care
Na ninaowatouch husema mshikaji
Uko smart upstairs
Usiache kuongea
Usiache we ni incharge huna spea
Kipaji ka' Ngwea, Kwa mpaji ni ka zawadi aliowagea

Flagi pepea
Alhitaji zaidi ya maji na mmea
Ilikuaje wamuache hadi mshikaji
Ulaji wa drugs ukamzoea
Tunamoka ili kusafiri kihisia
Au kufoka pia ikitoka ukaisikia
Huwezi ichoka au kuitosa  ikikuingia
Kinachoichosha  hiinia
Ni kosa ulichokiota kupatia
Kuwachota kihisia, tunasota
Je inatosha fidia

Shibe ya mdau hainilazi njaa
Sababu mganga yuko juu
Na furahaya baadhi wadau
Ni kimuona star wao anawalamba miguu
Asiye nihitaji simuhitaji
Kamwe simuachi aje azinzi
Bandidu kama Tsotsi sipigi goti ka PNC
Hakuna ambaye hakosi, labda zizi kwa dee andy
Yangu self-esteem haitoki ka ripoti za TMZ
Na hainizuii nisile mkate
Kwa kuhofia kiungulia
Na u-Emcee hauniachi, huniangalia kama fidelia
Kama Bruce Lee hizi karate, mtatupigia mtaishia

Na sintosita kusema ahsante au kuwasifia kwa kuinisaidia
Washkaji baadhi hawana haki
Ya kuipresha hii medula
Wako radhi kukupa pombe
Na sio pesa ya kula
Nawaona vyura tu kama Snura
Hii sura ya muhuni haina kwere
Masta mnaovaa masuti mtaani
Nyumbani kunguni tele

Kwa magonjwa yanayotibika tunayapoteza maisha huruma
Tunachanga kwenye msiba ukifa, hawajali ukiumwa
Au wanaweza wakahisi umekufa
Kwa kukutwa umezirai
Usipostuka Afrika
Unaweza kuzikwa ukiwa hai

Sumu! Sumu, Sumu
Sumu! Sumu, Sumu

Haumuui chura kwa kumtupa ndani ya maji
Ukinizuga kwa ulaji
Nitakupa fact kwa lugha ya kiushkaji
Mnataka vitu rahisi
Mie nawapa vitu halisi
Watata mnamtaka ibilisi
Na siyo bi kaka ka' Idris
Mr. Nice jua la utosi na mtaa una kiu ile mbaya
Hawamsapoti, isipokuwa wanawapromoti aliowainspaya
Wakati, ney sio kama moxie
Stoshi hakupaswa kumgwaya Lakini
Uzee bila noti ni zaidi ya Nyoshi akiwa vibaya
I didn't come this far, just to come this far
Siwezi sanda kama bikra hata nikiishi ki-star

Maisha hayakupi unachotaka ila yanakupa unachotafuta
Pesa sadaka, wazushi wanaivuta kwa chafu tatu
Binadamu wako wapi
Mnanitoa mie nsiwemo
Leo nawapa ofa ya mswaki
Halafu kesho mnaning'oa meno

Time is money nafasi haijali kukuzuga
Wema anataka saa ya almasi
Zari anaujali muda
Washa sana nyasi, rasta ogopa fast vuta
Wanashindwa kujinafasi kwa unafiki nafsi zinawasuta
Wabongo wa majuu hamna upendo, mnajigawa
Uongo hauna miguu lakini skendo zina mabawa
Aliyemtia umasikini Afrika leo analia kwa yanayomsibu
Na humtangaza akimpa masaada kiasi cha kumtia aibu
Dunia siyo chafu ni chafu uchafu tukiutazama
Sumu ndani ya watu, na ndiyo hapo hapo tunapokwama
Hawaamini kwenye kuunda Diamond au Kiba wawili
Wanachoamini ni kumshusha mmoja ili mmoja awe dili
Cha kupewa hakishibishi ukipewa lazima ukumbushwe
Dunia mwendo wa ngisi, kung'aa sio lazima star ashushwe
Ukiacha hisia zikuendeshe, kwa ujeuri utaishia kufeli
Sababu neno la ukweli sio zuri na neno zuri halina ukweli
Nitasahau vyote, milele nitamkumbuka aliyeniumba
Na daily nitakaa mkao wa push up tu kama umbwa

 

Watch Video

About Sumu

Album : Sumu (Single)
Release Year : 2020
Copyright : (c) Ngocha Wanene Entertainment
Added By : Afrika Lyrics
Published : Aug 17 , 2020

More FID Q Lyrics

Comments ( 0 )

No Comment yet



About AfrikaLyrics

Afrika Lyrics is the most diverse collection of African song lyrics and translations. Afrika Lyrics provides music lyrics from over 30 African countries and lyrics translations from over 10 African Languages into English and French

Follow Afrika Lyrics

© 2025, We Tell Africa Group Sarl