Imeisha (Outro) Lyrics
Imeisha (Outro) Lyrics by FID Q
We chali unaonekana una akili nyingi
Una miaka mingapi? "Mitano"
Enhe malizia huu msemo, mkono mtupu? "Haulambwi"
Safi mbili mara tano inakuwa ngapi? "Kumi"
Baba wa taifa ni nani? "Nyerere"
Na kama weupe ungekuwa mali?
"Ubuyu usingepakwa rangi"
Kumi mara kumi ngapi? "Mia"
Ukilia chakula ndani ya chungu itakuwaje?
"Harusi yako itakuwa na mvua"
Unachokifanya wanafanya watu wengi
Lakini wewe unaonekana uko bora kuliko wao
Hii inakuwa aje? "Inakuwa imeisha hivyo"
(Wanene)
Wanaonipigia niwape njia
Ndio wale walioamini sitoboi, mmepotea
Walioniona mlala hoi wakani-avoid
Kumbe sikukosea
Na wote wanaoniskia wanenjoy
Na siku hizi nimeendelea hadi mama ametulia
Niko so she is like boy boy
Endeleza mishe mishe tengeneza doh
Wezesha wasiojiweza ukitaka uwalishe
Wasilale fo fo
Zinduka chupa shuka kuwa bize usijishow show
Tafuta hadi wenye husta usijifiche
Wanarosto hao sipiti chocho zao
Wanavinyongo kwa nini mi ndo moto wao
Nikiwapa mchongo naona ka niko na shobo
Na nikitema nondo, nasema ana usonjo mwanao
Wabongo na wako na shombo zao na mauongo
Longo kaacha mkongo na bao
Sijui kasongo, kigongwa ka mombo wa kimombo
Waacha hongo waacha msondo, wacha jongo
And I'm the illest negro alive
Watch me prove it
Jitose chugu la loss au ku coach mafundi
Boss na ujuzi so choose mapozi na uzushi
Ku-force makuzi haitoshi ka una jozi lukuki
I rap with a cause, rebel by birth Rambo
You can't step on my shoes I'm Airforce babu
Wanaotest me wapuuzi wapokezi tush wangu
Siwezi mess na wanafunzi ambao wanashare ujuzi wangu
Wharap star, you know who you are
Wengine watakujudge unavyovaa
Mamangu huziba mdomo ili niepuke balaa
Ye mamake hamkatazi, coz she's the porn star
Aii imeisha iyoo, imeisha iyoo
Imeisha iyoo
Aii imeisha iyoo, imeisha iyoo
[Lordeyez]
I'm the last man standing kutoka kitaa changu
Last man standing kutoka kwa shule yangu
Natoka skuli nilikuwa mcat sikuwa mrat
Nice slice sleki ties sling
Ndo huyu nimeunda kwa mtaa
Walioona siendi mwenye nyumba wananishangaa
Afro misuko, kipara umetoga?
Enzi hizo ukisuka eti analiwa mboga
Jamani nimetoka mbali kulikuwaga hamna uboga
Ilikuwa kama ndoto na leo ndo nayaishi
Nikitazama nyuma nimepita kibishi bishi
Tumepoteza wanetu nao walifaa waishi
Mipango ya Mungu Baba haitofaa kuleta ubishi
Wapumzike kwa amani wanao bado tunaishi
Hamna uhakika wa kesho ila bado tunaishi
Tunahangaika sana hakuna asiye na mwalimu
Ninataka kubeba basi niyavae majukumu
Nguvu tunayo, nia tunayo
Basi uhakika bendera hio na ipepee
History tunazo, idea tunazo
Far bidi na Isaack hilo neno lipepee
Muipeperushe duniani je unajua jeje
Nalisha neno toka Africa, hamnaga siri
Hamnaga siri naweza fanana na hasidi
Nalisha neno toka jungle
Siku hizi naona mipango
Asimkufuru Mungu baadaye akazikwa kwa malengo
Aii imeisha iyoo, imeisha iyoo
Imeisha iyoo
Aii imeisha iyoo, imeisha iyoo
Imeisha iyoo, imeisha iyoo
Watch Video
About Imeisha (Outro)
More FID Q Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
You May also Like
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2025, We Tell Africa Group Sarl