MADEE Hadithi 2060 cover image

Hadithi 2060 Lyrics

Hadithi 2060 Lyrics by MADEE


Star from Mazoze Music Baby
Welcome to Dar es Salaam
It's Madee yoh, yeah

Mbili zero moja tano ulikuwa mwaka mzuri
Tukamchagua John Pombe Magufuli
Alifanya mazuri hako na sifa ka maduli
Alipiga vinduli wa madaraka kama nduli

Alipinga kuamka na hangover
Alichukia foleni za stopover
Akaanza Tazara kujenga ma treni over
Hey nigga huyu ndo over

Ulipo popote wana tunakupa tano
Na ikumbukwe ile ni awamu ya tano
Ilikuwa poa haijawahi kuboa
Na kama ulikosoa we mwenzetu ndo una doa

Ina maana haujawahi kupita pugu
Sawa haupandi wewe ina maana hauna ndugu
Baba ujugu wacha gubu
Njoo uone Manzese viberiti kama njugu

Hadithi, hadithi, hadithi
Tuhadithie
Hadithi, hadithi, hadithi
Tuhadithie

Hadithi yeah, hadithi, hadithi
Zile za kale 
Hadithi yeah, hadithi, hadithi
Za hapa kule na pale (Tuhadithie)

Tulipendaga sera zake kipindi anatuongoza
Asiyefanya kazi basi asile na ataoza
Mabulldozer walomchokoza 
Hawana kuta nzuri zaidi ya jela walioza

Aliitwa nani muite Pombe Magufuli
Mpenda amani tena maskini jeuri
Kazaliwa Chato mji mzuri kama Napoli
Na ukitaka sato sangara pia wapo

Mpenda amani rais wa wanyonge
Ah tena zamani walisoma bure kina chonge
Sikulipa fee mpaka namaliza chuo
Niliitwa Madee na nina hela wakati huo

Dunia ilimsifu, wanamziki walimsifu
Walimvika mataji ya kimila na kichifu
Huyo ndo rais wetu zile wakati huo
Haya wote mkalale kesho si mnakwenda chuo

Hadithi, hadithi, hadithi
Tuhadithie
Hadithi, hadithi, hadithi
Tuhadithie

Hadithi yeah, hadithi, hadithi
Zile za kale 
Hadithi yeah, hadithi, hadithi
Za hapa kule na pale (Tuhadithie)

Hata wizara zake kamwe hazikulala
Aweso wa maji, utalii kigwe gwala
Alikuwa ni mwenyekiti wa CC na M
Alitufanya na sisi tupende kila sehemu

Alikuwa ni mwana kwetu
Yeye kiongozi kwetu
Alikuwa ni mchizi wetu
Na alikuwa ni baba yetu
Huyu ni mwamba Magu kutoka Chato
Alikuwa ndo rais bora 
Ukipinga shauri yako

Hadithi, hadithi, hadithi
Tuhadithie
Hadithi, hadithi, hadithi
Tuhadithie

Hadithi yeah, hadithi, hadithi
Zile za kale 
Hadithi yeah, hadithi, hadithi
Za hapa kule na pale (Tuhadithie)

Watch Video

About Hadithi 2060

Album : Hadithi 2060 (Single)
Release Year : 2020
Copyright : (c) 2020
Added By : Huntyr Kelx
Published : Aug 18 , 2020

More MADEE Lyrics

MADEE
MADEE
MADEE

Comments ( 0 )

No Comment yetAbout AfrikaLyrics

Afrika Lyrics is the most diverse collection of African song lyrics and translations. Afrika Lyrics provides music lyrics from over 30 African countries and lyrics translations from over 10 African Languages into English and French

Follow Afrika Lyrics

© 2024, We Tell Africa Group Sarl