Huu ni Moto Lyrics
Huu ni Moto Lyrics by TANNAH
Tanna ft Bright - Huu ni moto lyrics
Naona mnachekesha, upepo mnaupaka rangi
Mnaweka siku kwenye friji na hazigandi
Mnapagawa eeh, njaa baada ya shibe
Mnakesha kupika mawe na mnangoja yaive
Sihitaji kuendesha gari
Endesheni nyinyi maana mimi naendesha
Akili za makaka mjini
Usipoiva, utaula mbichi
Kamata mwizi maana mie sikamatiki
Ngoja kwanza(Aaah) msinishike
Dhamani ya kuku mpaka sikukuu ifike
Pata potea najua hutanielewa
Ni kama mwiba ulikoingia utatokea
Pumzi ndogo njiani wamekomea
Leo mnavunja mwiko na jungu limekolea
Kwenye hii beat ni mazishi msibane
Msiba hauna gharama marehemu kafia nyumbani
Huu ni moto, wa kuotea mbali
Mtoko, na sitoweza haya
Ngoma ya kitoto, pole huwezi igiza kali
Jibebe, jibebe
Mwendo kasi natia gear
Ukianza namalizia
Ngoma lisambe spidi mia
Ukiunga tela nakanyagia(Ona)
Sasa ipi mnataka? Nini mnataka?
Huu mchezo mbona simple
Pumzi za mrisho ngasa
Tannah ni Tannah, wewe ni wewe
Ingiza vifaranga ndani nakatiza mwewe
Am the winner nimepangwa na vibonde
Mnatoka makamasi mnagongana ka vikombe
Mtaa wa ambapo, nibebe
Kinondoni Tannah, TMK ni Chege
Nitachezesha reggea nitawalewesha mbege
Mtaanza kuona moshi kama disco la reggea
Watoto mwisho mtatokaga damu
Mtajikuta posta mnaamkia sanamu
Tannah na Bear moto hauzimi
Majembe ya nini sasa? Na mjini hatulimi
Jua ina giza aisee mtapotea
Mi Tannah ni bahari mtajikuta mnaelea
Huu ni moto, wa kuotea mbali
Mtoko, na sitoweza haya
Ngoma ya kitoto, pole huwezi igiza kali
Jibebe, jibebe
Mwendo kasi natia gear
Ukianza namalizia
Ngoma lisambe spidi mia
Ukiunga tela nakanyagia(Ona)
1,2 - 1,2 mi ndio matawi ya juu
Level chafu, busu nasi
Mbona mtaa yalikuuma
Yaani sana tu, saana tu
Ushindi wa matuta kwenu afadhali
Namba saba kwenye bukta mjihadhari
Polepole bila pupa nawalaza chali
Kazi chobo chenga nawapiga dali
Zigizaga eeh, zigizaga
Nawashona zigizaga...
(Kiri Records)
Watch Video
About Huu ni Moto
More TANNAH Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2024, We Tell Africa Group Sarl