Tausi Lyrics by MRISHO MPOTO


Tausi wewee
Tausi wee
Karibu tausi uipambe nyumba yetu
Tausi wewee
Tausi wee
Mpendwa tausi kwa yangu mwana kwetu
Chanua mbawa zako (tausi)
Waiyone rangi yako (tausi)
Mpole sauti hiyo ndiyo sifa yako (tausi)
Chanua mbawa zako (tausi)
Waiyone rangi yako (tausi)
Jichunge tausi wasinyofee nyowa lako

Karibu tausi
Karibu sana tausi
Mchezo uliotukuta nao ni wa sadakalawe amina
Mwenye kupata apate mwenye kukosa akose
Kipo patiwa cha kuku kukali mweusi analiaje kwiyokwiyo
Mpaka lini mwenye kupata apate
Mpaka lini mwenye kukosa akose asante tausi
Umeukataa mlio wa kwiyo na rangi ya kuku kugawana
Tausi harufu unayo isikia ni ya chakula walichokula
Wameamua tu kujisaidia nyuma ya nyumba
Ii harufu irudi ndani kumchefua mpishi
Usishtuke ndivyo ilivyo kwa watu wenye shibe
Tausi umbo lenye kukataa huleta tumawe mawe
Unapotaka kututambulisa watoto wako kwa wageni
Tumia idadi yetu na sio ajira maana baadhi ya wanao wanatumia aka
Siku hizi watakufuga kumbuka njika la kuni ni fungato lilo
Fungwa kwa mkazo halipaswi kumumiza mubebaji
Karibu tausi

Tausi wewee
Tausi wee
Karibu tausi uipambe nyumba yetu
Tausi wewee
Tausi wee
Mpendwa tausi kwa yangu mwana kwetu
Chanua mbawa zako (tausi)
Waiyone rangi yako (tausi)
Mpole sauti hiyo ndiyo sifa yako (tausi)
Chanua mbawa zako (tausi)
Waiyone rangi yako (tausi)
Jichunge tausi wasinyofee nyowa lako

Tausi mimi mwanao baada ya kutoka jandoni
Nilidhani mimi ni mkubwa sasa naambiwa ooh
Icha kilichotolewa nikipande cha ngozi tu
Hakina mahusiano na kukua kwako
Kweli ina maana kila anaye ingiza kidole puani
Ana mashaka na alicho nusa uliwai kusema we mwenyewe mnyonge
Hapigani kwa fedha na tulifanya makosa kuchagua silaha
Silaha tulio ichaguwa inatutia unyonge na kuondowa unyonge
Kwa kutumia silaha ya wenye nguvu ambazo sisi hatuna
Tunazidi kupoteka muda muda huu
Wa sisi kukua au nyakati
Tausi nimeamini asie ona anakutumia
Jucho usiku sio kwa ajiri yake
Anawamulikia wanao ona ili wasimkanyage
Nah ii hii yote tausi lazima ioze
Kila mwenye zamu yake asiwache kumwagilia

Viroboto kupe huretaga virusi tausi
Ukuta mweupe wasiufanye mweusi tausi

Tausi wewee
Tausi wee
Karibu tausi uipambe nyumba yetu
Tausi wewee
Tausi wee
Mpendwa tausi kwa yangu mwana kwetu
Chanua mbawa zako (tausi)
Waiyone rangi yako (tausi)
Mpole sauti hiyo ndiyo sifa yako (tausi)
Chanua mbawa zako (tausi)
Waiyone rangi yako (tausi)
Jichunge tausi wasinyofee nyowa lako

Watch Video

About Tausi

Album : Tausi (Single)
Release Year : 2022
Added By : Farida
Published : Jan 11 , 2022

More MRISHO MPOTO Lyrics

MRISHO MPOTO
MRISHO MPOTO

Comments ( 0 )

No Comment yet



About AfrikaLyrics

Afrika Lyrics is the most diverse collection of African song lyrics and translations. Afrika Lyrics provides music lyrics from over 30 African countries and lyrics translations from over 10 African Languages into English and French

Follow Afrika Lyrics

© 2024, We Tell Africa Group Sarl