Paradiso Lyrics
Paradiso Lyrics by STAMINA
Tuonane paradiso
Tuonane paradiso
Tuonane oh paradiso
Tuonane paradiso
Najua wengi mnaumia mtu akiwa hoi mahututi
Kila nafsi ni ulimi lazima itaonja mauti
Wengi wenu dah mnalia kinafiki
Mnasahau kwamba mshahara wa dhambi
Haulipagwi benki ndugu
Najua mnakuwa wengi msibani
Ila kipindi cha wacha ajabu mbona hatuonani
Moyo wangu unaniuma sana ila wacha nibaki bubu
Bora kidonda rafiki kuliko kidonda ndugu
Ila presenter anaongea kama anajua
Wakati nishamuomba interview mara kibao na akazingua
Na ndo maana sikutoaga rushwa kwa dj
Nilijua tu nikifa mtapiga bure bila pay
Nishapeleka nyota yangu kwa waganga mara ngapi?
Ushanisimanga kwa maneno hadi ukachoka kiko wapi
Binadamu aliyekamilika haya nionyeshe yuko wapi
Kama malipo duniani sema nikulipe shingapi
Mshaniteka, mkanitesa mkanifanya mnachotaka
Mshanifunga hadi jela bila hatia kisa mamlaka
Usinyanyase haki ya nani nakwambia
Na wote mnaotembea leo hii ni marehemu watarajiwa
Wanaolia hawahesabiki
Ijapo hawakunipenda zamani
Wanafiki leo marafiki
Hawana hata haya usoni
Wanasubiri mpaka nife
Ndo sifa zangu zije ziskike
Mmeniwekea mashada ambayo siwezi hata kuyanusa
Jeneza la bei ghali ambalo siwezi hata kuligusa
Mmepika hadi waba ambao siwezi hata kuonja
Wakati hamkuleta matunda kipindi nilipokuwa mgonjwa
Rafiki wa kweli ni yupi?
Anayekunyenyua wakati unaanguka
Hawa anahakikisha anakuangusha unapoinuka
Maana rafiki wa karibu waliniona kama mzigo
Ungenipa moyo inatosha si lazima wanipe figo
Wasanii wezangu jau, nadhani mshasahau
Nishatuma sana macover hamkuposti
Au mlitaka dau, leo nimekufa ndo mnaposti
Vipi mnangoja nije nikomenti au
Boss nilifanya kazi kubwa na hukunipa mshahara wangu
Na bado ukaona haitoshi ukatembea na mke wangu
Ukaleta simanzi mpaka kwa watoto wangu
Nashangaa leo unamwanga machozi kwenye msiba wangu
Nimeona rambirambi ya rais, hivi kaileta nani
Najua yuko busy kuwashinda kambi ya upinzani
Ningekuwa hai ningemfanyia hata kampeni
Kazi ya Mungu haina makosa, wote tuseme AMEN
Wanaolia hawahesabiki
Ijapo hawakunipenda zamani
Wanafiki leo marafiki
Hawana hata haya usoni
Wanasubiri mpaka nife
Ndo sifa zangu zije ziskike
Bora uzikwe ukiwa hai
Kuliko kuishi kwenye dunia
Wanatamani ukatishwe uhai
Japo usoni wanakuchekea
Binadamu, hawa binadamu
Binadamu wouwooo...
Wanaolia hawahesabiki
Ijapo hawakunipenda zamani
Wanafiki leo marafiki
Hawana hata haya usoni
Wanasubiri mpaka nife
Ndo sifa zangu zije ziskike
Watch Video
About Paradiso
More STAMINA Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
You May also Like
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2024, We Tell Africa Group Sarl