Baba Lyrics
Baba Lyrics by STAMINA
Kwanza naomba ukae chini alafu uvute pumzi
Nina vitu vya kuongea ambavyo najua vitakuudhi
Hivi unajua nimekuvumilia sana
Angekuwa mtoto mwingine tayari ungeshampa laana
Najiuliza sijui nikuseme na kipi baba
Najiuliza sijui nianze na lipi labda
Mama anasema mwanzo mimba ulikataa
Kwanini sasa hukutoa ukaruhusu mpaka akazaa?
Alafu hivi hauzijui kinga
Haukujua pekupeku kama italeta mimba
Uchi wako wa kijinga ndo saa hivi unanitesa
Usingemrubuni mama labda angemuoa bakresa
Dah, unanipa kiwewe
Au manesi walichanganya babangu haukuwa ni wewe
Kama unataka kunipiga we yote sawa
Au nikuchumie fimbo unichape kisawa sawa
Hata kama ni mzazi
Saa zingine nawaza nikuchukie
Sema tu we ni mzazi
Acha ukweli wako nikwambie
Daddy iii, naongea na wewe eh
Daddy iii, naongea na wewe
Naongea na wewe
Ile hela ya kuhonga ungetoa ka sadaka
Mungu angekubariki ungenizaa kama baraka
Ukajichanganya kaisari ukampa hisiaka
Alafu mbele ya Yesu Petro ukampa mamlaka
Mbona Mzee Mushi namuona na hela
Mzee Mwakalinga mwenzio ana hela
Mzee Luta Shobwa ndo kabisa na mihela
Wewe ulikuwa wapi mpaka unakufa kabwela
Nikuulize, ukifa nitaridhi nini?
Labda jina la ukoo alafu linisaidie nini?
Utajiri hivi haukuona kwanini
Maana pombe unazokunywa siwezi ridhi hadi maini
Umeshindwa hata kununua kiwanja
Ona mpaka leo tupo nyumba za kupanga
Elimu siku hizi ni bure
Ila cha ajabu umeshindwa kunipeleka shule
Inauma sana ila acha tu nikuulize
Ina maana ujana wako umeshindwa kuwa busy
Nikiendelea kuongea naona kama nitakufuru
Nakuombea kwa Mungu akupe nuru
Hata kama ni mzazi
Saa zingine nawaza nikuchukie
Sema tu we ni mzazi
Acha ukweli wako nikwambie
Daddy iii, naongea na wewe eh
Daddy iii, naongea na wewe
Naongea na wewe
[Professor Jay]
Mwanangu nimekuskia nakuombea kuwa uyaone
Nilijua umekuja kwangu kuniombea ili nipone
Kumbe umekuja na shari kunilaumu na kunihukumu
Inaonyesha ningesinzia ungeninywesha hata sumu
Baada ya ujauzito wako tulipima na mamako
DNA ilionyesha kuwa mimi sio damu yako
Ukiskia ukubwa hujalala basi jua dunia ni dambo
Nikasimama kidete kupigania maisha yako
Tena nilingoja ngoja ukue
Nikajitoa kwa hali na mali ili usijue
Nikafanya mambo mengi hatari ili nikutunze
Wakanisweka jela ili dunia inifunze
Ukuwaji wako sidhani ulilishwa mila
Nilipambana kila kona kuwataftia ngawila
Niliuza mali zangu ilimradi wewe usome
Leo unanipandishia kibase nyambavu tena unikome
Mwone mtoto wa Sobo, mwenzio ni rubani
Mtoto wa Sugu juzi kapata udiwani
Mtoto wa Bwire ndo daktari marekani
Hebu toa bangi zako, aliyekuambia usisome nani?
Hata kama ni mzazi
Saa zingine nawaza nikuchukie
Sema tu we ni mzazi
Acha ukweli wako nikwambie
Daddy iii, naongea na wewe eh
Daddy iii, naongea na wewe
Naongea na wewe
Hata kama ni mzazi
Saa zingine nawaza nikuchukie
Sema tu we ni mzazi
Acha ukweli wako nikwambie
Daddy iii, naongea na wewe eh
Daddy iii, naongea na wewe
Naongea na wewe
Watch Video
About Baba
More STAMINA Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
You May also Like
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2025, We Tell Africa Group Sarl