Wakati Wangu Ni Lini Lyrics

SIFAELI MWABUKA Tanzanie | Gospel,

Wakati Wangu Ni Lini Lyrics


Ninajiuliza sana 
Ninajiuliza kila siku
Wakati wangu ni lini? 
Wakati wangu ni lini?

Ninajiuliza sana 
Ninajiuliza kila siku
Wakati wangu ni lini? 
Wakati wangu ni lini? Eeh

Wakati wa kukutana na wewe
Wakati wa kuona mkono wako
Wakati wa kuona baraka zangu
Wakati wa kuinuliwa na mimi

Wakati wangu ni lini? 
Wakati wangu ni lini?
Baba niambie eeh

Niambie ni lini Baba(Baba niambie)
Niambie ni lini Mungu wangu(Nimechoka kulia)
Niambie ni lini Baba(Niambie, Baba niambie)
Niambie ni lini Mungu wangu(Wakati wangu ni lini?)
Niambie ni lini Baba(Baba nikumbuke)
Niambie ni lini Mungu wangu, eeeh

Ni wengi wamesema
Subira huvuta heri
Tena nimesikia 
Mvumilivu hula mbivu

Hezekia, alikuita Mungu wangu
Nawe ulimsikia Baba
Ulipotuma mtumishi wako, aende
Atengeneze mambo ya nyumbani mwake

Ukamwambia bwana
Ndipo Hezekiah akageuka
Akakuita Mungu wangu
Nawe ukamsikia Baba

Nawe ukamjibu Mungu wangu
Wakati wangu ni lini nami
Wakati wangu ni lini nami
Baba niambie...

Niambie ni lini Baba(Baba niambie)
Niambie ni lini Mungu wangu(Nimechoka kulia)
Niambie ni lini Baba(Niambie, Baba niambie)
Niambie ni lini Mungu wangu(Wakati wangu ni lini?)
Niambie ni lini Baba(Baba nikumbuke)
Niambie ni lini Mungu wangu, eeeh

Uniambie ni lini Baba
Uniambie ni lini Mungu wangu
Uniambie ni lini Baba
Uniambie ni lini Mungu wangu
Uniambieni lini Baba
Uniambie ni lini Mungu wangu, eeeh

Leave a Comment