Anaitwa Roma Lyrics
Anaitwa Roma Lyrics by ROMA
Anaitwa Roma hakuna wa kumstopisha Roma Roma
Nani wa kunyamazisha Roma Roma
Kazi kuongea ongea kesho yake on air
Kesho kutwa wamepotea
Anaitwa Roma hakuna wa kumstopisha
Nani wa kunyamazisha Roma Roma
Kazi kuongea ongea kesho yake on air
Kesho kutwa wamepotea
Wanauliza siku hizi Roma huimbi za kiharakati
Huku wakisema ununio ndo kumbukumbu iliyo baki
Ahh sasa hamtaki mbona hamkumsapoti Mange
Nyinyi mtakuwa wanafki yaani sijui mlikwama wapi
Walivunja dole la mwisho wakaliacha dole la kati(Mmh)
Eeeh hii si ni nchi ya demokrasi mkimind basi mnajua
Sa mbona kamati(Mmmm) Tuiache hayo
Vipi korosho za Mtwara
Maana wapiga kura wengi wakulima wafanya biashara
Kumnyima mpinzani ajenda, tendetu yaliyo mema
Sio kumpelekea defender mtaani tutie vilema
Chozi ya waTanganyika hayatawaacha salama
Na damu zilizo mwagika milele zitawaandama
Serikali imewapa nafasi wanawake pongezi ifike
Najiona mwenye bahati nikimtazama mwanangu wa kike
Akikuwa akiuliza wale waloniteka nani aliwatuma
Mjibuni mmemzaa mpare ila asiwachukie wasukuma
Najua atanuna najua ya nyuma yatamtia huruma
Asilipe kisasi ashtaki kwa Mungu aipate suna
Na nikiitwa kwa Mungu Baba nikafa
Sijamuona mtoto, mmpe shada la msalaba
Aliweke upande wangu wa kushoto
Na mtapo imaliza ibada iwe ni padi ya paroko
Nguo zangu azipige mnada mmpe albino ama uroko
Mi ni soja niko vitani
Nikipona unikiss silaha nawaachia maishani
Ibebeni mkomboe taifa maana nchi yenu itaangamia
Viongozi hawana maarifa na hawataki wakosolewe
Wanafanya kazi kwa sifa
Anaitwa Roma hakuna wa kumstopisha Roma Roma
Nani wa kunyamazisha Roma Roma
Kazi kuongea ongea kesho yake on air
Kesho kutwa wamepotea
Anaitwa Roma hakuna wa kumstopisha
Nani wa kunyamazisha Roma Roma
Kazi kuongea ongea kesho yake on air
Kesho kutwa wamepotea
Yuda usimharibie Dani ili ufurahishe mtukufu
Sisi wote wanao kwanini unapenda sana Yusufu?
Yakobo, baba pesa madaraka umaarufu
Wanaomwapata vijana wanakosa hekima na utu
Wapunguzie vifungo wafungwa wasio na hatia
Wengine walifuata mkungo kiukweli hawakuwa na nia
Naskia jimbo la Ubungo kuna mtu amelipania
We umezitungo ni zaidi ya waraka wa Waibrania
Chama kilisha watimua na siasa mlowanunua
Mnapiga bomu mortuary mnajisifu mmeua
Tuliombee taifa tuombee viongozi wetu
Nchi ina miiba so tuwavishe viatu walioko peku
Tusilete uchama kwenye issue za kitaifa
Uongozi ni kuacha alama chanya na kuajibika
Kutekana kuuana sio sifa ya MTanganyika
Ubora ndama ndio unalipa zizi la ng'ombe uhakika
Hongera baba kwa ukusanyaji wa mapato kedekede
Ya kodi na flyover ndio hizo kanyaga twende
Kwetu huduma ya afya ni bora kuliko ndege
Atafanya yote tumuombee na tuimbe Yesu nibebe
Watu wametumbuliwa mwezi mmoja kabla ya kustaafu
Walimu wamesahauliwa mapato yao halafu
Mapolisi mishahara yao bado twapiga tafu
Hospitali boresha tupunguze idadi ya wafu
Anaitwa Roma hakuna wa kumstopisha Roma Roma
Nani wa kunyamazisha Roma Roma
Kazi kuongea ongea kesho yake on air
Kesho kutwa wamepotea
Anaitwa Roma hakuna wa kumstopisha
Nani wa kunyamazisha Roma Roma
Kazi kuongea ongea kesho yake on air
Kesho kutwa wamepotea
Sijawai kuona mpga kinanda wa kanisa akitoa sadaka
Cameraman akianguka ndani ya misa kwa pepo kaka
Na sadaka halali ni ile utaitoa kwa uchungu
Tafta pesa wee siku hizi hulijali sio ukubwa rungu
Na nyota mshale we bishoo segera
Ukuki na kulenga tokea hale
Nenda kalete mamluki karoge mambo iko huku
Roma anaiteka show, kafara unamchinjia kuku?
Mi namchinja naichinja kondoo
Andaa show alafu mmlete mkali wenu tafta venue
Baada ya dakika mbili mpige mziki ya maiti yenu
Eti unarap? Huwa unarap wewe? Unarap nini?
Ni wanakubeba na hautaamini usiku wakikupiga chini
Sa we kamatia chini mi nakamatia ndinga
Na ukikamatia mpini si utakamatia mimba
Alafu kizazi nakwacha unang'aza sharubu
Kula nganzi mi kisirani nina gubu
Na elfu mbili na ishirini si tumwombe Mungu
Wewe na mimi na wote wasaka tonge watao rudi vitini
Watuepushe na hiki kikombe mwaskizisha nguma pini
Mjengoni wasikae kinyonge
Anaitwa Roma hakuna wa kumstopisha Roma Roma
Nani wa kunyamazisha Roma Roma
Kazi kuongea ongea kesho yake on air
Kesho kutwa wamepotea
Anaitwa Roma hakuna wa kumstopisha
Nani wa kunyamazisha Roma Roma
Kazi kuongea ongea kesho yake on air
Kesho kutwa wamepotea
Watch Video
About Anaitwa Roma
More ROMA Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
You May also Like
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2025, We Tell Africa Group Sarl