Interview Lyrics
Interview Lyrics by RAPCHA
Asubuhi flani ya hang over bwii
Nani tena huyu ananipigia saa hii
Napapasa kuitafuta simu mpaka naikamata
Macho kwenye screen naona jina “GACHI B”
We mshezi una balaa hatari
Sjui zilikua ni tungi au vijiti walimix wale
Uliwaka ukavamia dem wa mtu ukamshika shika
Na ukawa unaforce kumkiss eti palepale
Nlijua lazma utani-roast
Sjawahi waka vile mpaka ikatokea hadi data zime-lost
Mchizi alinitwika ngumi bufff kwenye mdomo yani
nkahisi nmepoteza meno yote on the spot
Usingeweza kutoboa pale
Ilibidi ncheki gap tuchomoke tukimbie mbali
Nlikudrop kwako ukanambia nkushtue mapema
Una interview ya kazi leo katafte ugali
Ayaaa nahisi nshachelewa
Duhh mchongo bado nusu saa nkichelewa hawatonielewa
Umetisha kunishtua acha niwahi chap nkawaskie
nikitoka ntadondoka studio oyeah
Haya
Mswaki dakika moja, kuoga dakika moja
Suruali ya kitambaa imejikunja na iko moja
Ila haya yote ningeandaa tangu jana isingekua
kazi fresh nitanyoosha daika moja
Naboost simu isinizimikie nkiwa njiani
Muda unaenda sana sa inabidi ntoke ndani
Navaa chap uber njoo nifate sinza vatcani
Sina muda wakuelekeza fata ramani
Dakika mbili uber akafika
Madevera smart kama wewe mjini ndo wanahitajika
Skia Nirushe chap posta pale 99 plaza ntakuongeza buku 5 tukiwahi kufika
Palepale kwanza dreva kawaka
Daah leo ka bahati yani mzee wa lissa nimekunyaka
Hivi kwenye ule wimbo ulipigwa kweli?
Sioni hata makovu na ile story vipi ishakukuta kweli!??
Sasa hapa ndo tutapochelewa
Focus yako iwe kwenye kuniwahisha na sio kuongea
Mgenilipa kama mnavyonisifia
Saivi nsingekua busy kutafuta kazi nisiyoielewa
Hii ndo shida ya wasanii bongo
Mbele ya camera wapole sana na kujisifia uongo
Mnasema mnatupenda mashabiki
Ila tunapokutana mnatutreat kama vile tunanuka shombo
Na ndo shida ya mashabiki wa bongo
Mnapenda tu kupuuzia ukweli na kuamini uongo
Mnasahau ka na si ni binadamu kuna muda tuna stress zetu mtuvumilie kidogo
Muda unaishia afu bado kuna umbali
Nikamlipa dreva nikashuka kwenye gari
Psss psss boda niwahishe posta chap tu
Zimebaki dakika 5 ufike muda wa interview
Mbio mbio mpaka destination
Zimebaki dakika mbili tu afu mchiz ndo naingia reception
Dada wa mapokezi akafurahi aliponiona
Si akataka alete story nkaona ananichoma
Nkiwa palepale reception
Najibizana huyu sista, haki nimechoshwa na questions
Wakaingia watu wawili ndani
Yule dada alivyowasalimia ikabidi nkae attention
Nageuka nione kuna nani
Ndo namuona yule dada ambae jana nilimfata nkamletea uhuni
Pembeni yake kaongozana na mumewe alieyataka kunitoa meno na ndio boss wa kampuni
Ilinichukua ka nusu sekunde kukumbuka ule uzito wa ile ngumi kwenye lile tukio
Nkakamata bahasha ya vyeti vyangu kwa makini nkatazama
Mlango ulipo vvvuuum nkatimua mbio
Watch Video
About Interview
More RAPCHA Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
You May also Like
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2025, We Tell Africa Group Sarl