Nionyeshe Lyrics by Q CHILLA

Oooh mapenzi
Oooh, eeh mapenzi

Meli ishaweka nanga
Usiwape taabu waganga
Eti uniroge
Ya kazi gani?

Zinga kipande cha kanga
Uje tulicheze vanga
Kisha nikoge
Unikande mabegani

Mmmh
I wish uone moyo wangu
Ulivyojawa makovu
Huenda utanionea huruma

Nahisi we ndo dawa yangu
Umeshushwa mwokovu
Nisikumbuke ya nyuma

Hey
Mwenzako nishapitia mikasa
Drama kila wakati
Shahidi yangu mwenyezi

Mmmh
Hadi nikahisi nina nyota ya tasa
Ama sina bahati
Aah katika mapenzi

Basi nionyeshe
Nionyeshe! Unavyonipenda mwaya
Nionyeshe! Unavyonipenda mwaya
Nionyeshe! Mmh unavyonipenda mwaya 
Nionyeshe! Walonitenda mpaka waone haya

Mmmh
Jichunge na peji za udaku
Yasemwayo ni ya uwongo
Akina Mange kimambi

Ogopa na manyaku nyaku
Mahodari waongo
Wasije kuweka kambi

Nikipata tule wote
Nikikosa utangoja, richwa tulale
Wasikutishe chochote 
Waso isha vihoja vichwa kambale 

Nikianguka niokote
Tusimame pamoja sare sare
Hadi tuzikwe sote
Utoge ndonya ukongoje mmakonde chale

Mmmh
I wish uone moyo wangu
Ulivyojawa makovu
Huenda utanionea huruma

Nahisi we ndo dawa yangu
Umeshushwa mwokovu
Nisikumbuke ya nyuma

Basi nionyeshe
Nionyeshe! Unavyonipenda mwaya
Nionyeshe! Unavyonipenda mwaya
Nionyeshe! Mmh unavyonipenda mwaya 
Nionyeshe! Walonitenda mpaka waone haya

Oooh my God its Spencer

Music Video
About this Song
Album : The Return of Chilla (EP),
Release Year : 2019
Copyright : (c) 2018 WCB WASAFI
Added By: Huntyr Kelx
Published: Jul 23 , 2019
More Lyrics By Q CHILLA
Comments ( 1 )
.
1884 2020-04-28 23:27:50

Cool