Nataka Kutoka Lyrics
Nataka Kutoka Lyrics by NIKKI MBISHI
Bro nataka kutoka
Unataka kutoka kwani wewe mwari?
Bro nisaidie nami nataka kutoka
(Tongwe Records) Toka hapa!
Nitoke vipi?
Bwana misosi akatoka
Hmm ila Alikiba hajatoka
Japo kuna mida ukiingia unamkosa
Anaingia anatoka, anaingia anatoka
Wewe ambaye unataka kutoja hujamuona?
Diamond hajatoka, hujaskia ana ngoma
Anavyo wakanyaga sijui nani atapona
Na Tanasha ana kibendi, ila mi sijakiona
Sijui hikio kibemi, ni lini kitatoka
Na akitoka tutaona ka ni simba au ni nyoka
Unataka kutoka kwani we mwari?
Unataka kutoka bro ulikuwa ndani?Watu bwana
Ng'ang'ania ng'ang'ania mlango utakubana
Joh Makini si kaka ako, katokea ala
Ye na Fid Q wote bado sana
Hawajawai kutoka wapo wapo sana
AY hajatoka, FA hajatoka
Roma hajatoka, Vee Money hajatoka
Nakushangaa wewe bana unataka kutoka
Bro nataka kutoka
Unataka kutoka kwani wewe mwari?
Bro nisaidie nami nataka kutoka
Haya toka hapa!
Nani mwingine anayetaka kutoka
Anyooshe kidole nimtoe
Nani mwingine anayetaka kutoka
Anyooshe kidole nimtoe
Walitest kumwendea simba, kumshika wakashindwa
Akawa boss wa redio na kituo cha runinga, anavimba
Watoto wacha kupiga mayowe, kufuatana DM
(Bro una kipaji, naomba unitoe)
Nyie madogo mnachekesha kweli kweli
Mnawaza kutoka kabla kuingia
Hamjifunzi kuwa tufsia aliyetoka
Kwa sababu ya ulofa
Mnaenda ikizagaa zawadi ya unyota eeh
Mwisho inakuwa unyoka, unyama unyamani
Hudai fair play kwenye unyang'anyo
Ubishi unasaidia, ndio maana sitoki
Nang'ang'ana sing'oki, kufanana usifosi
MB Doggy ametoka
Mr Nice ametoka
Ferooz ametoka
Fathe sele ametoka
Inasemekana eti kwenye game wamechoka
Wanaotaka kutoka fuateni hizo ndoto
Mnazi ota
Bro nataka kutoka
Unataka kutoka kwani wewe mwari?
Bro nisaidie nami nataka kutoka
Haya toka hapa!
Nani mwingine anayetaka kutoka
Anyooshe kidole nimtoe
Nani mwingine anayetaka kutoka
Anyooshe kidole nimtoe
Watch Video
About Nataka Kutoka
More NIKKI MBISHI Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2024, We Tell Africa Group Sarl