Maneno ya Mashabiki Lyrics
Maneno ya Mashabiki Lyrics by NIKKI MBISHI
Nikki Mbishi ana chuki ana wivu ana gubu
Mziki umemshinda hana kitu anatubu
Anaishi chumba kimoja anajitia kiburi sugu
Fid alisema hana nidhamu mithili ya wile wadudu
Stress zimemjaa ye ni pombe tu na ndumu
Game imebadilika ye anakomaa tu na ngumu
Tv zimemchoka na redio zimemtosa
Anaposti tu mashairi kweli soko limemnyoosha
Wenzake wanapiga mchele kimya kimya bila kwere
Wana magari tele na majumba kama Mbere
Kazi yake kuponda ponda hana fact wala mantic
Anaota kuna siku ata-sign iwa na Atlantic
Anajidai mjuaji hapendwi hana washikaji
Hana tuzo wala taji nini Benzi ama Bajaji
Kifupi jamaa mzugaji, mamluki msindikizaji
Anakuletea uzushi anadai uhai ni maji
Ni mashabiki, wanavyosema
Mziki umemkimbiza anahema
Hata kiki hapati tena
Pabaya panamwita hataki pema
Ni mashabiki, wanavyosema
Mziki umemkimbiza anahema
Hata kiki hapati tena
Pabaya panamwita hataki pema
Alijifanya anaacha mziki njaa ikazidi akarudi
Anadiss kupata kiki hapo ndipo anapo bugi
Kipaji Mungu kambariki tatizo hafanyi juhudi
Ukimwambia ukweli anakublock hana budi
Anaita wenzio ma-whack
Redioni hana hata hit song
Nahisi anavuta unga
Maana ana ushikaji na King Kong
Ruki mwenyewe hasikiki si apige ngoma na Ringtone
Abbah na Mr T Touch wanaotawala kingdom
Japo duction inapunguza harakati
Mziki umejaa corruption na yeye rushwa hataki
Wenzake wanaachia ngoma zinatrend kwenye chati
Wengi wanatake over kwake haplay ya manati
Haendi na wakati ana swagga pale kati
Umri umezidi kwenda na ametengwa na kamati
Anaendekeza jenga sijui atajenga wapi
Anashindwa na Dogo Njanja sababu anapenda unafiki
Ni mashabiki, wanavyosema
Mziki umemkimbiza anahema
Hata kiki hapati tena
Pabaya panamwita hataki pema
Ni mashabiki, wanavyosema
Mziki umemkimbiza anahema
Hata kiki hapati tena
Pabaya panamwita hataki pema
Ukiacha sauti ya jogoo
Hana tena album kali
Video zake zote mbovu
Wenzake wanaskika mbali
Mziki umemwacha chali siku hizi anauza mistari
Tangu enzi za JK haalikwi taftari ya ikulu
Itakuwa vipi usawa huu wa Magu?
Sanaa haimlipi hata aseme aende kwa babu
Anajiona special wakati maajabu hana
Asipofanya commercial atapata taabu sana
Maana kipigo chake ni zaidi ya Mr Nice
Jinsi alivyofulia hapati hata Insta likes
Akitaka tumkubali, ajipange aje tena
La sivyo hasikiki tena hadi Mange akisema
Aache bangi akitema hapo brand ataijenga
Apate manzi kama Nandy amfanye ka Bill Nenga
Nikki mbishi, Nikki mbishi kitu gani
Wenzako wamewasha more fire hamwoni kitu hewani
Ni mashabiki, wanavyosema
Mziki umemkimbiza anahema
Hata kiki hapati tena
Pabaya panamwita hataki pema
Ni mashabiki, wanavyosema
Mziki umemkimbiza anahema
Hata kiki hapati tena
Pabaya panamwita hataki pema
Watch Video
About Maneno ya Mashabiki
More NIKKI MBISHI Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
You May also Like
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2024, We Tell Africa Group Sarl