NACHA Why Always Me cover image

Why Always Me Lyrics

Why Always Me Lyrics by NACHA


Ladies and gentleman
I go by the name N.A.C.H.A
A.K.A Nacha
Nyasubi ndani ya mbany baby
Why always me
Moment of silence

Unemployment numbers ni nyingi skuizi
Thus why mitaa imepambwa na a lot of university degrees
Na kinachoniumiza ni kuona degree holders wakisaka kazi
Na wenye kazi ambayo inahitaji degree hawana degree hio ndio kazi
Excuse me

Si wenyewe watoto wa kimaskini tu
Tunategemea jasho letu ili tuishi
Na tunategemewa ukiomba tusipate
Tuharibikiwe walo nyuma yetu vipi wataishi
Why always me?
Na maisha yamekuwa kama sport betting
Unaweka over, yenyewe yanatoa under
Na ulikuwa unangoja cash out
Ndio utabaki unashangaa kama
Kumkuta mwenyeji akilala gesti house
But so far so good, sie hatujawahi kushindwa
Sema tu muda wa kushinda ndio haujafika
Am telling you hata huyo mpenzi unaemficha kama pincode za benzi
Wahuni wanakesha wakipull table, wakiingiza white dent
The time unareply text ya girlfriend wako huku unashangilia
Ndo time anatuma text huku akiwa na mwanaume mwingine akamlalia
Na mafanzi hawaijui industry but nawashukuruu wana apriciate
Nachokifanya wanasema nisiache wanapata shule
OK fine but budlack wanaishia
Kunipea sifa ambazo kimsingi kazinifanyi mimi nile
Inanikera coz the furure is now, yani sasa naahaata
Nikipigana kuwa jambo kubwa la sasa but still industry inaniita the next big thing
Nimeshasubiri sana, now nimechoka ku trust the process
Why always me?
Si tunazisaka ndoto kipindi nyie mnasaka usingizi wa pono
Darasani nlikuwa namba one but sa hii namba one kwenye life ni Yule
Aliefeli shule akashikwa mkono kipendacho roho hula nyama mbichi na mi sina nyama
So namshangaa mpenzi wangu akiniomba tu meet
Why always me?
Kuutafuta urijali kwa kumeza vidonge unajitesa
Urijali ni kuwa na pesa kipindi mnaendekeza uzinzi na uasherati
Kipindi mnautilia masjaka uchumba wa nandy na billnas
Ndo kipindi mi niko zangu tandika nikiuza miguu ya kuku
Kashata na kai mati nikijenga future yangu mambo ya kipuuzi mi staki
Yani ujinga ujinga ujinga naweka pendi
Nyie akili zkiwaza vijora zikatwerk jangwani sea breeze wikend
Mi nikimuwaza mke wangu niliemuacha nyasubi anakibendi
Kila nkiwaza watoto wangu, wazazi wangu najijuta naheshimu musa na pesa
Kama smenti na maji yanavyoheshimiwa na mjenzi
Why always me?
Nimeamini maisha bila unafki hayasongi tambua hilo
Ni kama sheikh anaekemea maovu afu wikendi tunapiga nae
Gambe na ndudu kilo
Astachafilullha
Let me tell you something

Kuapgrade majendo ya shule halafu tusiupgrade mishahara ya walimu
Hatupigi hatua maboresho ya miundo mbinu yanaenda sambamba
Na maboresho ya tumbo kaa ukijua yani bila , Kazi hakuna kushiba na bila
Kushiba hakuna kazi so it’s a win win situation
I make sense nyinyi kula ndani halafu mnatoka nje kututangazia tuwe wavumilivu
Katika kipindi hiki kigumu tumekumbwa na ukata mnatutia mashaka
Usinipige, usinipige, usinipige
Nakwambia na wala usinionee
Mimi na wewe tuko sawa mbele ya sheria
Na hio ndio demokrasia
Mmeamua kuchagua pesa over utu na sio, utu over pesa
Na ndio maana nasisitiza umakini unahitajika sana
Umakini unahitajika sana kipindi ambacho hujifanya bata
Na samba hujifanya kuku najua bado hujanipata
Umakini unahitajika sana
Umakini unahitajika sana kipindi chan kufanya matendo ya kiungwana
Wakati ni mfungua masufuria yani paka
Umakini unahitajika sana najua bado hujanipata
Hapa naongelea kiti yani madaraka na sikuhizi mkaidi hafaidi siku ya idi tu
Anafaida hata pasaka najua hujanipata ok
Ondoa shaka nachojua sijatukana
Nitakuelewesha nilimaanisha nini siku nyingine muda nikipata
Why always me?
Football, I love you so much football
Tanzania football federation tunaacha legacy ipi kwafaida ya inayokuja generation
Uongozi ni dhamana,
Yes, ten asana na ndomana achene wadau watoe maoni yao
Heunda tukajenga kupitia mawazo yao
Yana maanahaina haja ya kudhalilishana na kufungiana
Mpira nni uwekezaji nut mkiamini uwekezaji ndio mpira tunafeli
Mnakosea na siasa za usimba na uyanga ndio zinaathiri wawekezaji
Kutokea clubs zinaendeshwa kupitia mifuko ya wadau halafu mnasema club
Ni tajiri na mashabiki hawaamini matokea ni sayansi ya kiwanjani wannamini
Matokeo ni mzee mpili waamuzi wetu mtawalaumu bure tu maslahi yao
Hayakidhi mahitaji ya kijamii na wataendelea kudanganya tu hata
Mkiweka msaada wa video assistant referee
National team players tunakula nao chipsi kwa sele bonge
Na tunagombania nao madem usiku element
Bado tu unajiuliza ni kwanini wachezaji wetu chapa zao ni kubwa
Na hawapati endorsement??
Njia pekee ya kuwapunguza marafiki ni kuwatangazia kuwa una shida
Sihitaji marafiki wanaongoja nipate pesa wajipande
Getto kwangu kama sofaset wala sihitaji marafiki ambao vichwa
Vinawaza mzinga havina positive mindset
Why always me?
Nawaona mnavostrago kumfanya nzi atengeneze asali
Hio kazi naiweza mimi nyuki pekee ipo siku ntapaa angani kama
Kunguru mkiwa chini yangu niwanyee
Bongo mbona hupewi attention kwenye redio na TV
Wakati mwaka jana ulifanyiwa mahojiano mpaka na BBC
Why always me?
Hapo ulipo ni baba na upo kwa baba una ngoja ule asubuhi ukiamka
Uwahi kijiweni ukabishane nani mkali kati ya John book na fiston mayele
Nitadili nao perpendicular yani jino kwa jino
Na mnapompandisha twaha kiduku please msimshushe mwakinyo
Tupongezane panapostahili kupongezana na tukosoana panapostahili kukosoana
Daraja la salenda, ongezeko la shule miradi mingi tu imejengwa
Maslahi ya wasanii mirabaha ndo ya msingi tulipofika so pabaya
Kiukweli unapigwa mwingi
Niamini, mnajua nini ?
Sababu za kibaiolojia ndio zimefanya nacha awe tofauti na nyinyi
Yes na hii ni kwa wote mnaoniskiza take notice msiache kuonja mboga
Even chumvi kamiksi laiza

Watch Video

About Why Always Me

Album : Why Always Me (Single)
Release Year : 2022
Copyright : © 2022 channel administered by ngomma vas
Added By : Farida
Published : Apr 05 , 2022

More NACHA Lyrics

NACHA
NACHA
NACHA
NACHA

Comments ( 0 )

No Comment yetAbout AfrikaLyrics

Afrika Lyrics is the most diverse collection of African song lyrics and translations. Afrika Lyrics provides music lyrics from over 30 African countries and lyrics translations from over 10 African Languages into English and French

Follow Afrika Lyrics

© 2024, We Tell Africa Group Sarl