Hodi Lyrics
Hodi Lyrics by NACHA
Hodi wenyewe Nacha ndo nagonga
Namuulizia ndoa hivi nimemkuta au katoka
Ala kumbe yupo mwite namhitaji huku
Naitaka sana ndoa ila tatizo najishuku
Nataka kujua pia nimekuja kukuuliza
Na kama ndoa ni tamu ni kwanini inawaliza?
Ni kwanini inawaumiza bado najiuliza
Na ni kwanini baada ya ndoa majuto hupitiliza
Wanandoa wengi hawana furaha
Na wengi wao mara nyingi tunakutana sana bar
Nakata tamaa jirani kila siku zogo
Na na mbona wanandoa wengi wana nyumba ndogo?
Kipi ni sababu ya wanandoa kugombana?
Kitandani hana kipya kwaiyo hana tena maana?
Aliamua kukuigizia na kuwa kakupenda sana
Au mlikurupuka kipindi cha uchumba nyinyi mkaoana
Inanipa wasi inaniwia vigumu
Kuamini nikioa ndoa yangu inaweza dumu
Mawazo yananikumba nikiwaza kuingia ndoa
Nachohofia ni kuingia ule mlango wa kutoka
Hata maji ya moto kuna muda yanapoa
Hakuna kitu kibaya kama kukosea kuoa
Sorry kwa usumbufu ila nilitaka tu nipime
Nitarudi tena wacha nigonge hodi kwingine
I'm coming home
Nakuja nilivyo, kichwani kiulizo
Coming home, waambie
Milango yote inanikataa
Acha nijaribu siasa majitaka taka
Dini kabisa hofu napata pata
Ndoa kabisa imenikataa
Ngoja nigonge mlango wa dini nitatue haya mafumnbo
Nijue kinagaubaga sitaki kufuata mkumbo
Mi sio Isaka, Yakobpo wala Musa mwenye fimbo
Wanafanya kwa faida ya Mungu au faida ya matumbo?
Nijitie mkosi na nijisahau
Na mwisho nikapige goti chini mbele ya madhabahu
Au nijivike ugaidi ukaidi hayawani
Au niwe na busara kama mfalme Suleimani
Mlango nyeti hadi kuingia tu naogopa
Mnanishauri niji Macca au mchungaji wa kuokoka
Nikiingia huku kuna vitu nitavikosa
Starehe za kidunia unadhani wapi nitapata?
Mmenipata? Na nacho ogopa
Ni kumjaribu Mungu kwa kuingia na kutoka
Nimkane kama Petro nimsaliti kama Yudah
Niutangaze ufalme wa Mungu mbele yao nikiwa shuhuda
Niingie kupata pesa 'NO' moto utanichoma
Au niingie kuitangaza injili kila kona
Toa ndugu toa, toa ulichonacho
Ninunue Prado mpya nongeze kipato
Ogopa kuwa Mungu wakati we mwenyewe una Mungu
Siku Mungu akikasirika dunia utaiona chungu
Kuabudiwa kama Mungu na unajua we sio Mungu
Ni kutafuta mchawi nani na unajua mchawi ndugu
I'm coming home
Nakuja nilivyo, kichwani kiulizo
Coming home, waambie
Milango yote inanikataa
Acha nijaribu siasa majitaka taka
Dini kabisa hofu napata pata
Ndoa kabisa imenikataa
Kila mlango ni mgumu sioni pakukimbilia
Najiuliza kwanin ni lazima ndani mi kuingia
Kabla sija ghairi nakuna kichwa faster
Nawaza nikagonge labda mlango wa siasa
Naskia ni mchezo mchafu sitaiweza mi ni msafi
Naogopa kulaghai watu mwisho wakipati
Naogopa tega ndoano niwavue hawa samaki
Na mwisho nishibe mimi niwanyime wao haki
Au niingie huenda naeza kuwa bora ka Nyerere
Bora ka Mandela nifikishe nchi mbele
Nikifa nikazikwe kwa shujaa Butiama
Au kaburi langu likazikwe Nyasubi Kahama
Kabla sijaingia kuna vingi niliona
Kura za haki bao la mkono Maradona
Kwa Mungu sasa nitachosema nini?
Ikiwa nilikula nikasaza nikasahau walio chini
Siasa ina makali kama kisu
Nikikumbuka alivyotakaga kuuawa
Nafikiria kutekana nafikiria kuchafuana
Na ndicho naogopa sana
I'm coming home
Nakuja nilivyo, kichwani kiulizo
Coming home, waambie
Milango yote inanikataa
Acha nijaribu siasa majitaka taka
Dini kabisa hofu napata pata
Ndoa kabisa imenikataa
Watch Video
About Hodi
More NACHA Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
You May also Like
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2024, We Tell Africa Group Sarl