MARTHA MWAIPAJA Naiona Kesho cover image

Naiona Kesho Lyrics

Naiona Kesho Lyrics by MARTHA MWAIPAJA


Naiona kesho kesho Iliyopangwa na baba
Naiona kesho kesho Iliyopangwa na Mungu
Naiona kesho mimi kesho iliyopangwa na baba
Kesho ya heshima aah Iliyopangwa na baba
kesho ya Neema iliyopangwa na baba
Kesho yenye utukufu iliyopangwa na Baba
kesho ya kuinuliwa iliyopangwa na baba
Kesho ya ushindi ii iliyopangwa na Mungu
Kesho yenye nguvu iliyopangwa na baba

Sitaki kuitazama Leo yangu mwenzenu
Sitaki kuitazama Leo yangu mwenzenu
Leo yangu ni shida mwenzenu
Leo yangu ni tabu mwenzenu
Leo machozi yanitoka aah mwenzenu
Leo nimekataliwa aah mwenzenu
Leo nimefukuzwa mapema mwenzenu
Leo wote waniacha aah mwenzenu
Leo machozi ni mengi hii mwenzenu

Sitaki kuitazama leo yangu kamwe
Sitaki kuitazama leo yangu mimi
Leo yangu ninalia mwenzenu
Leo ninateseka aah mwenzenu
Leo mateso ni mengi hii mwenzenu

Naiona kesho yangu mwenzenu
Naiona kesho yangu mwenzenu

Japo vita yangu ni kubwa mwenzenu
Maadui wangu ni wengi mwenzenu
Japo mateso yangu ni magumu mwenzenu
Kuna neno amesema nami mwenzenu
Atapigana aah amesema
Atafanya mlango ooh amesema
Atanifanyia wepesi amesema

Japo vita yangu kubwa mwenzenu
Japo adui ni wengi mwenzenu
Japo njia siioni mwenzenu
Atapigana mwenyewe amesema
Atafanya wepesi iiih amesema
Atanifanyia wepesi kwani amesema
Atanichunga salama mh amesema
Atafanya mlango ooh amesema
Atapigana na adui aah amesema
Kasema niione kesho aliyoniwekea
Kasema niione kesho aliyoniwekea

Kuna majira yalifika nikajua mungu
Kuna majira yalifika nikamwelewa
Majira Yale yalikuwa magumu
Majira Yale yalikuwa magumu
Kwa macho yangu nikaona akitenda
Kwa macho yangu nikaona akitenda
Akasema mwanangu nakupenda
Akasema mwanangu nakupenda
Usiitazame Leo yako mwanangu
Usiitazame Leo yako mwanangu
Mbona mimi ni Mungu nikupendaye
Mbona mimi ni Mungu nikupendaye

Ni kweli kwa macho ya nyama mimi nimechoka
wengi wanitazamapo kweli nimeshindwa
Wengi wanionavyo kweli nimeshindwa
Kweli kwa mbio za mimi nimechoka
Kweli kwa mwendo wangu nimeshindwa
Kwa macho ya nyama nimechoka
Kwa macho ya watu nimeshindwa

Lakini hakuna hata mmoja
Anayejua Patano langu na Mungu
Lakini hakuna hata mmoja
anayejua nimepatana nini
Tumepatana na Baba hataniacha
Hata nikisukwa sukwa sitamuacha
Hata nikilia nisimuache
Hata nikiteseka aah nisimwache
Tumepatana na baba
Nimepatana na baba

Nimepatana na baba
Nimepatana na baba
Naiona kesho yangu iliyonjema haa
Naiona kesho iliyonjema haa 
Mwenzenu Naionaaaa kesho

Naiona kesho kesho iliyopangwa na baba (Kesho ya heshima)
Naiona kesho kesho iliyopangwa na Mungu (Kesho ya Neema)
Naiona kesho kesho iliyopangwa na baba (Kesho ya kufanikiwa)
Kesho ya heshima aah, kesho ya utukufu iliyopangwa na baba
Kesho ya heshima (Ya heshima yangu na Mimi)
Iliyopangwa na mungu (kesho ya wote kumjua Mungu wanguuu)
Kesho ya heshima iliyopangwa na baba

Naiona kesho kesho iliyopangwa na Mungu (Kesho ya Neema)
Naiona kesho kesho iliyopangwa na baba (Kesho ya heshima)
Naiona kesho kesho iliyopangwa na baba (Kumjua Mungu wanguuu)
Kesho ya heshima aah, iliyopangwa na baba (Kesho)
Kesho ya ushindi aah, iliyopangwa na Mungu (Kesho)
Kesho ya heshima aah, iliyopangwa na baba (Kesho ya heshima, Kesho)

Watch Video

About Naiona Kesho

Album : Naiona Kesho (Single)
Release Year : 2021
Copyright : (c) 2021
Added By : Huntyr Kelx
Published : Nov 09 , 2021

More MARTHA MWAIPAJA Lyrics

MARTHA MWAIPAJA
MARTHA MWAIPAJA
MARTHA MWAIPAJA
MARTHA MWAIPAJA

Comments ( 0 )

No Comment yet



About AfrikaLyrics

Afrika Lyrics is the most diverse collection of African song lyrics and translations. Afrika Lyrics provides music lyrics from over 30 African countries and lyrics translations from over 10 African Languages into English and French

Follow Afrika Lyrics

© 2024, We Tell Africa Group Sarl