LOMODO Namaanisha cover image

Namaanisha Lyrics

Namaanisha Lyrics by LOMODO


Iyee, mmmmh
Naahidi nitakupenda mpaka kifo
Kitutenganishe 
Tuvuke majangwa na mafuriko

Kwenye baridi 
Wewe ndo wangu jiko
Acha kuni nichochee 
Unanipa joto

Eh sema utakacho mie sawa
Sitabishana
Waseme utakavyo mie chawa
Tukiongozana

We ndo wangu paracetamol
Watuliza maumivu ya moyo
Sina mwingine oooh ma yoo

Na maneno yasiyozidi kimo
Yakaleta gharika ya moyo
Wasitukalie vikao

Namaanisha, ninamaanisha
Namaanisha, ninamaanisha

Na nikisema nakupenda
Basi ujue namaanisha
Chizi mto kwa midenda
Kwa verse natiririka

Ooh baby mi mwenzako 
Nimezama vibaya yaya
Sijiwezi 
Usinitupe ukamakaya yaya

Nisipokuona mi roho juu juu
Nikikuona tu napata nafuu
Sitaki kuota njia ni wewe tu
Harufu manukato we ndo karafuu

Na kama tiba 
We ndo wangu paracetamol 
Watuliza maumivu ya moyo
Sina mwingine ooh ma yoo

Na maneno yasiyozidi kimo
Yakaleta gharika ya moyo
Wasitukalie vikao

Namaanisha, ninamaanisha
Namaanisha, ninamaanisha

Watch Video

About Namaanisha

Album : Namaanisha (Single)
Release Year : 2020
Copyright : (c) 2020
Added By : Huntyr Kelx
Published : Aug 11 , 2020

More LOMODO Lyrics

LOMODO
LOMODO
LOMODO
LOMODO

Comments ( 0 )

No Comment yetAbout AfrikaLyrics

Afrika Lyrics is the most diverse collection of African song lyrics and translations. Afrika Lyrics provides music lyrics from over 30 African countries and lyrics translations from over 10 African Languages into English and French

Follow Afrika Lyrics

© 2024, We Tell Africa Group Sarl