Deni Lyrics by LINEX SUNDAY MJEDA


Utavuna ulichopanda
Mama mi ni mdeni wako
Natembea nina deni lako
Kwenye moyo

Sijajisahau 
Mama mi mdeni wako
Namuomba Mungu nikulipe
Kipindi cha uhai wako

Utavuna ulichopanda
Mama mi ni mdeni wako
Natembea nina deni lako
Kwenye moyo

Nakuta mtu kaposti picha
Kawajengea wazazi wake
Maisha yao kayabadilisha
Machozi amewafuuta

Haimanishi sikuwazii, mama
Fanya subira mwanao 
Bado nipo Dar es Salam 
Napambana

Kazi ngumu imekuwa 
Ni sehemu ya maisha yako, mama
Ushike jembe ukalime 
Ndo upate, iwe ni ya, kula yako

Haimanishi sikuwazii, mama
Usivunjike moyo wakati wangu upo

Utavuna ulichopanda
Mama mi ni mdeni wako
Natembea nina deni lako
Kwenye moyo

Sijajisahau 
Mama mi mdeni wako
Namuomba Mungu nikulipe
Kipindi cha uhai wako

Utavuna ulichopanda
Mama mi ni mdeni wako
Natembea nina deni lako
Kwenye moyo

Sijajisahau polisi 
Waliochukua kidogo ulicho nacho
Enzi nyumbani tunauza ngongo
Nawakumbuka mpaka sura zao

Mama Sandra uko kwenye moyo wangu
Fikira zangu We ndo maisha yangu
Nitakufuta machozi na jasho 
Ulilotoa tokea nikiwa tumboni mwako

Nilikadamiwa nikiwa kichanga
Maskini ya Mungu sina hata dhambi
Ninawashukuru wazazi wako mama 
Kwa kutupa kambi

Na siwezi kukufuru
Nimeshasamehe nilimwachia Mungu
Haimanishi sikuwazii, mama
Usivunjike moyo wakati wangu upo

Utavuna ulichopanda
Mama mi ni mdeni wako
Natembea nina deni lako
Kwenye moyo

Sijajisahau 
Mama mi mdeni wako
Namuomba Mungu nikulipe
Kipindi cha uhai wako

Utavuna ulichopanda
Mama mi ni mdeni wako
Natembea nina deni lako
Kwenye moyo

Watch Video

About Deni

Album : Deni (Single)
Release Year : 2019
Copyright : All rights to the owner.
Added By : Huntyr Kelx
Published : Jul 09 , 2019

More LINEX SUNDAY MJEDA Lyrics

LINEX SUNDAY MJEDA
LINEX SUNDAY MJEDA
LINEX SUNDAY MJEDA
LINEX SUNDAY MJEDA

Comments ( 0 )

No Comment yetAbout AfrikaLyrics

Afrika Lyrics is the most diverse collection of African song lyrics and translations. Afrika Lyrics provides music lyrics from over 30 African countries and lyrics translations from over 10 African Languages into English and French

Follow Afrika Lyrics

© 2024, We Tell Africa Group Sarl