Corona Lyrics
Corona Lyrics by LAVA LAVA
(Banny Music)
Ee Mola waja wako tumesimama
Tuonyeshe suluhisho
Kutwa tumeshika tama
Hatuishi masikitiko
Ama hizi ndo zile zama
Ziloandikwa za mwisho
Oooh mtoto analia baba mama
Wote manung'uniko
Nilidhani utani wanatudanganya
Waongo nikawaona, nikawaona
Si unajua vijana wa maskani, wajuaji sana
Eti Bongo hakuna Corona, Corona
Mara kitimu timu
Nasikia habari, kila nikipita
Waziri Umi mwalimu
Katangaza tayari, kuna waadhirika
Makundi kundi matimu
Tamko la serekali, marufuku kukusanyika
Ukanipata wazimu
Nitapata wapi ugali? Show zote zimevunjika
Mmmh sekondari, primary
Na vyuo vyote vifungwe
Ukiona una mbaya dalili
Muone doctor usivunge
Eeh hili ngojwa hatari
Kabisa tujichunge
Usije ukafanya siri
Itakuua
Corona, corona eeh! Unataka nini?
Corona, corona eeh! Kwetu umefuata nini?
Corona, corona eeh! Umekosea nini?
Corona, corona eeh! Utaondoka lini?
Moyo umetanda hofu
Masikini mimi
Ndugu zangu walotoka Europe
Wote wako karantini
Ishamkumba SK, wasi wangu Salam
Na yule Mwana FA, washaposti Instagram
(Sorry, naomba kurudia kidogo)
(Kipande hiki kimenihuzunisha sana)
Ishamkumba SK, wasi wangu Salam
Na yule Mwana FA, washaposti Instagram
Eeh na sasa Wasafi kweupe
Hakuna watu ofisini
Naona marupe rupe
Jamani tuwe makini
Mmmh sekondari, primary
Na vyuo vyote vifungwe
Ukiona una mbaya dalili
Muone doctor usiunge
Eeh hili ngojwa hatari
Kabisa tujichunge
Usije ukafanya siri
Itakuua
Corona, corona eeh! Unataka nini?
Corona, corona eeh! Kwetu umefuata nini?
Corona, corona eeh! Umekosea nini?
Corona, corona eeh! Utaondoka lini?
Mikono kwa sabuni, osha osha
Kwa sekunde ishirini, osha osha
Vaa mask usilete uhuni, osha osha
Ukiwa nyumbani ofisini, osha osha
(In God We Trust)
Watch Video
About Corona
More LAVA LAVA Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
You May also Like
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2024, We Tell Africa Group Sarl