Nimwage Radhi by HARMONIZE Lyrics

Alilililiiii
Ayo lazier

Furaha isio kifani, kumpata mwandani
Hakika wamependeza, Ngoma lipo uwanjani
Kaibiwa Nani, sa unaachaje kucheza

Hama kweli harusi imefana, Tena ya kihistoria,
Na hii ndio message Sema na mumeo usifate ya jirani

Pande zote baba na mama, Naona wanashangilia
Ila sitaki kua mnafki, Jumba bovu kuniangukia
Nina langu la moyoni, ningependa kuwaambia
Bi harusi, mashoga wakupupia, Hao niwakuwaangalia
Wako wale wahali gani, wanakuja kuchungulia
Uwaombe samahani, uwakomeshe wambea
Eti, wifi umepika nini, na mimi utanigaia
Waambie, wamepika p dagaa, zenye pilipili nyingi
Zakutisha we na mumeo, wao watakimbia
Aiiii shemeji ndugu yo mumeo, usisikilize ya fulani
Na hii ndio message Sema na mumeo usifate ya jirani

Kwa Furaha niliyo nayo,
Niacheni nimwage radhi,
MI nataka nimwage radhi.
Ai yoi yooo
Niacheni nimwage radhi
MI nataka nimwage radhi
Alilililiiii

Ng'ombe anapoita ndama, tunasema kua analia
Kupigwa na kulalama, hatujawahi kusikia
Hakika mmependeza
Ninavyomfahamu Biharusi, sipati kusimulia
Nimetoka Ruvuma, Mchomori, namtumbo,
Lindi, mtwara mpaka chitohori nimezisikia
Sifa za binti huyu, Mola amemjalia
Binti hapendi majungu, Hakika ninawaambia
Ukimuazia viatu na gauni,
Anakuachia
Bwana harusi tunakupa mke, ukaishi nae vyema nyumbani
Huna kitu usimfiche mwambie, taabani
Ikiwezekana mkakope, mkono uende kinywani
Usimpige mateke, kisingizio kitu fulani
Ooh
Umefanya nini Jana, hakuliki leo ndani
Mtoto bado mteke, usimkomaze Kwa ngumi
Ukimshindwa mrudishe, kwao hajaua huyu
Mumeo akienda kazini, akirudi salimia
Wala usikae chini, chakula kumsukumia
Bali mkaribishe ndani, Hali kumjulia
Muulize za kazini, Kwa tabasamu muruua
Kisha msindikize bafuni, hata kama anapajua
Halafu wewe tafuta kiti, jikoni kimbilia
Chukua simu yako message, ukimtumia
Mwambie
Hasilani bila wewe, chakula hakitaingia
Eh
Aiiii shemeji ndugu yo mumeo usisikilize ya fulani
Na hii ndio message Sema na mumeo usifate ya jirani

Kwa Furaha niliyo nayo
Niacheni nimwage, radhi
Alilililiiii

Music Video
About this Song
Album : Nimwage Radhi (Single),
Release Year : 2018
Copyright : ©2018 Wasafi Records
Added By: Trendy Sushi
Published: Feb 09,2020
More Lyrics By HARMONIZE
Comments ( 0 )
No Comments
Leave a comment
Top Lyrics


You May also Like


Download Mobile App

© 2020, New Africa Media Sarl

Follow Afrika Lyrics