Boya Lyrics
Boya Lyrics by HANSTONE
Ulinifanya kichwa nazi boga
Akili ukaichanganya
Mapenzi niliyaweka wazi uroda
Ukaniona sina maana
Na ukanifanya ninyenyekee mama
Ati kufa tufe wote
Mapenzi sio rob ati nijaze kibaba
Nikianguka niokote
Kwangu ikawa mapenzi upofu
Na kwako sioni
Usikubaliki mithili ya jokofu
Nitalala na nani mama?
Tafadhali naomba, sitaki niache
Hata ukiniona wapi tema mate
Maana penzi langu lote nilikupa mi fire
Ila bado ukaniona mi, boya
Kama mtoto kanidanganya, boya
Zangu ndoto ukanizizima, boya
Kwa bedi sitoi boko umenijaa kichina, fire
Ati mtoko tutoke dinner, boya
Kumbe urembo si upake hinna, boya
Kwa wiko fimbo mzizi ndo shina, boya
Mmmh tiba ya tiba ya mapenzi sio hosipitali
Na toka lini kahawa ukaona imewekwa sukari
Ulinichanganya akili yangu ukaivuruga
Eti sina maana, toka mbele yangu unapoteza muda
Uliapa nitakufa nawe
Mpaka mwisho nitazikwa nawe
Ukanifanya mimi nipagawe
Mama mama mama mama
Ati saa hivi imebaki ndoto ndoto
Kubembelezwa ka katoto toto
Kwenye baridi nikupe joto
Utahadidhiwa
Saa hivi penzi latokota, toko toko
Usukani kulia au kushoto
Mambo ya Pwani ni kanga moto
Naogelea
Tafadhali naomba, sitaki niache
Hata ukiniona wapi tema mate
Maana penzi langu lote nilikupa mi fire
Ila bado ukaniona mi, boya
Kama mtoto kanidanganya, boya
Zangu ndoto ukanizizima, boya
Kwa bedi sitoi boko umenijaa kichina, fire
Ati mtoko tutoke dinner, boya
Kumbe urembo si upake hinna, boya
Kwa wiko fimbo mzizi ndo shina, boya
Watch Video
About Boya
More lyrics from Amaizing album
More HANSTONE Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
You May also Like
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2025, We Tell Africa Group Sarl