Mafanikio Lyrics by FID Q


[INTRO]
Kila mtu anataka mafanikio..

[VERSE 1: Fid Q]
Kujisikia nipo juu mie sitaki hizo deals
Sipendi makuu hivyo nitabaki kuwa real..
Na kila track ya Q aaah,.. Ni wazi utaifeel
Ni wazi iko full aah MZAZI ninakill
Ninamwagika kama Masika..
ninaheshimika na sio kanjibai
Kwa huu mziki wa bajaji hadi kwa washkaji wenye macadillac
Unawashika ile kibabylon.. Unauzika sana maghetoni
Ilimradi tu wawe happy more..midadi tu ila party noooo
Mkisinzia mtaniudhi nishawapa vyeo
Tuwape wapuuzi waliodai hii haiuzi haya matokeo
Safari ni hatua.. Kufika inabidi uianze
Haina kukita au kusita.. Inabidi ukaze
Ingia, ongoza au fuata njia, kukimbia ni mwiko
Kuanzia ulipo sio sawa na kubakia ulipo
Nikisema 'chini hapana' nina maana fanya unyanyuke
Na ukiamini umesimama mwana.. Komaa usianguke
Ukijituma na neema inakaribia..
Nyuma walio-give up mapema wangekaza wangeifikia
Penye... Happy.. Jitusu.. Unafki usiuruhusu
Yajue ya kuzingatia ili uachane na yasiyokuhusu
Kibongobongo longolongo shazi
Endelea kusaka mchongo hata ukipata kazi

[HOOK: Barakah The Prince]
Tunachukiana? Ndio..
Ila sio sababu kuacha riadha ya mafanikio
Ongeza mbio
Sababu kila mtu, kila kona anasaka mafanikio
Haukungoji wakati.. Ooh wewe
Zinapita nyakati..ooh  wewe
Muda wako bahati.. Oh wewe

[VERSE 2: Fid Q]
Na kughairisha kisa haupati sapoti
Ni kujificha na kuuliza giza.. Iko wapi ile tochi?
Haupati ile noti
Na wakati wa ule uboss ushapotea
Hautaki ukose? Usiache ofcoz endelea
Utafanikiwa kwa unachojua au unachofanya
Wachache ndio hutusua kwa jinsi tu wanavyoonekana
Mafanikio hayaji ukikata tamaa..
Yenyewe huwafuata wanaojituma na wale wasiosukumwa na njaa
Sipigi kila dili mipaka imezingatiwa
Sitaki kuwa tajiri ninataka kufanikiwa
Ili kuheshimiwa kwanza ni lazima ujiheshimu
Lakini kufanikiwa ni maujanja tu sio lazima elimu
Ili kuyadaka wengine hugeuka wabaya
Mafanikio kwenye kuyasaka wengine hugeuka malaya
Hugeuka was(i)o haya
Kutwa utawakuta kwa babu
Na anayefanya mambo ya maana huwa hana muda wa kuyahesabu
Kwenye kuyasaka hakikisha haufilisiki
Haupotezi maisha au vile vitu havinunuliki
Sio kama hatucheki kwasababu tumezeeka?
Nope.. Ni tunazeeka kwasababu hatujawahi cheka

[HOOK: Barakah the Prince]
Tunachukiana? Ndio..
Ila sio sababu kuacha riadha ya mafanikio
Ongeza mbio
Sababu kila mtu, kila kona anasaka mafanikio
Haukungoji wakati.. Ooh wewe
Zinapita nyakati..ooh  wewe
Muda wako bahati.. Oh wewe
Utumie basi... Eeeh eeeh

[BRIDGE]
Una mpenzi (na) uko lonely?
Im sorry ndugu.. Haujafanikiwa
Maisha ni kama boli, magoli ndio kufanikiwa

Oooh ooh oooh..oooh.. Ndio kufanikiwa
Kila mtu anataka mafanikio...

[OUTRO]
Hhhmmm.. Hhhhmmm.. Oh mafanikio
Oh mafanikio
Kila mtu anataka mafanikio

 

Watch Video

About Mafanikio

Album : Mafanikio (Single)
Release Year : 2019
Added By : Afrika Lyrics
Published : Jan 20 , 2019

More FID Q Lyrics

Comments ( 0 )

No Comment yet



About AfrikaLyrics

Afrika Lyrics is the most diverse collection of African song lyrics and translations. Afrika Lyrics provides music lyrics from over 30 African countries and lyrics translations from over 10 African Languages into English and French

Follow Afrika Lyrics

© 2025, We Tell Africa Group Sarl