DULLA MAKABILA Magufuli Dua cover image

Magufuli Dua Lyrics

Magufuli Dua Lyrics by DULLA MAKABILA


Haya wabitakabali dua, amina
Oooh Yarabi itikia dua amina
Aah Magufuli takabali dua, amina
Aah CCM itikia dua, amina

Wee kila siku naomba dua
Nchi wasichukue wapinzani
Na namuombea Magufuli
Asiondoke madarakani

Najua maadui wengi sana
Mola mpe nguvu ya kupambana
Anayoyafanya yanaonekana
Hio ndo zawadi yetu kwa Maulana

Kaboresha huduma za afya 
Mijini mpaka vijijini
We barabara usiseme 
Lami mpaka barazani

Ah mtendahaki asobagua
Tajiri wala masikini
Ah ningeweza ningemuombea 
Atawale miaka thelathini

Aah basi CCM takabali dua
Wee Magufuli itikia dua
Samia Suu takabali dua
Kassim Majaliwa itikia dua

Philip Mangula takabali dua
Wee Dr Bashiru itikia dua
Jamani Pole Pole takabali dua
Jamani Makonda

Dua lilijibu wacha niseme
Kawakomboa na wanawake
Wenye biashara kawapa mitaji
Magufuli pongezi kwake zifike

Dua lijaishia hapo
Wakuzembea ukakunja ndita
Na mafisadi ukawafurumusha
Air Tanzania ukadondosha

Dua likafika ufukweni
Sasa tuna meli kama mbele
Likafika hadi shuleni 
Wanafunzi elimu bure

Dua lifike kaburini
Alipolala mwalimu Nyerere
Ajue kaliacha jembe
Alolinoa kipindi kile

Aah basi CCM takabali dua
Wee Magufuli itikia dua
Samia Suu takabali dua
Kassim Majaliwa itikia dua

Philip Mangula takabali dua
Wee Dr Bashiru itikia dua
Jamani Pole Pole takabali dua
Jamani Makonda

Wanangu nani mwenye camera
Anipige mafoto
Mkubwa Fela nani mwenye camera
Achukue video

Nauliza nani nani? Nani 
Wee babu Tale nani nani? Nani nani
K Money nani nani? Nani 
Wee Dulla Tale nani nani? Nani nani

Kelele ya kwanza kwa Makonda yake (Weee)
Kelele ya pili kwa Samia Suluhu yake (Weee, weee)
Kelele ya tatu kwa Magufuli yake (Weee, wee, wee)

Waitee...
Basi twende piga makofi piga..
Piga makofi piga makofi CCM

Wee atarudi mmoja mmoja alosaliti chama
Wee atarudi mmoja mmoja alosaliti chama ma
CCM niwaambie, niwaeleze
Wanangu niwaambie, niwaeleze

We kura zote kwa CCM 
Wapinzani tunapiga chini
We kura zote kwa Magufuli
Wapinzani tunapiga chini

Wanangu mnasikia kelele hizoo
Wanakuuliza kuna nini?
Wapinzani wanaiba kura

Wee Magufuli anafanya kweli 
Wengine wanauza sura
Magufuli kipenzi chetu
Umepita bila kugombea

Ndio maana Pierre anapiga kura
Huku mkononi anabia
Ndio maana Pierre anapiga kura
Huku mkononi anabia

CCM si mlisema, aah si mliongea
Jamani si mlisema, aah si mliongea
Nikija Makabila, nyi mpaka nguo mtavua
Nikiimba Makabila, nyi mpaka nguo mtavua

Basi twende vua mashati vua, mtuonyeshe vifua
Vua mashati vua, mtuonyeshe
Ah wanangu vua mashati vua, mtuonyeshe vifua
Vua mashati vua, mtuonyeshe

Nasema woyooo, woyooo, woyoo
Aah CCM woyooo, woyooo, woyoo
Wen donki wangu wachezeshe mwanangu
Chapa!

Watch Video

About Magufuli Dua

Album : Magufuli Dua (Single)
Release Year : 2020
Copyright : (c) 2020
Added By : Huntyr Kelx
Published : Jul 10 , 2020

More DULLA MAKABILA Lyrics

DULLA MAKABILA
DULLA MAKABILA
DULLA MAKABILA
DULLA MAKABILA

Comments ( 0 )

No Comment yetAbout AfrikaLyrics

Afrika Lyrics is the most diverse collection of African song lyrics and translations. Afrika Lyrics provides music lyrics from over 30 African countries and lyrics translations from over 10 African Languages into English and French

Follow Afrika Lyrics

© 2024, We Tell Africa Group Sarl