Mlemavu Lyrics by DIZASTA VINA


Yeah!!  Haujui wimbo ulio bora dhahiri
Haujui ushairi au mstari ukaukariri
Haujui giza haujui baridi
Au mbu walonighasi wakati nakusubiri
Haujui kupenda, moyo wako hewa
Wote tumejifunza ila mwenzangu umechelewa
Kaa kimya hauna hata haki ya kusema
Upuuzi unaofanya sio ushujaa ni ukilema
Natamani upate ki-mista pengine
Kikuumize kama ulivo’waumiza wengine
Unaumwa mama hata kwa matibabu hautopona
Sio dhahabu naijua dhahabu nikiiona
Kuvimba kwako kamwe hakutavunja miamba
Ipo siku utajua kuwa kuringa si afya
Utatafuta upendo na utazikuta siasa
Utaelewa inavyouma pindi unapofanywa wa ziada
Kutojibu jumbe za simu sijui ndio kula njama
Kudanganya mahali ulipo umeshavuka zama
Huu ushenzi ni uzamani upo nyuma mama
Unapodhani ni ujanja nakuonea huruma sana
Eti  Queen, Queen hawezi choropoa mimba
Ungekufa kwa ngoma kinachokuokoa kinga
Unajirusha sana itakukatikia Kamba
Utazubaa na uzee utakukutia njiapanda
Unanuka sana unanitia kichefuchefu
Nimepoteza muda umenirudisha nyuma stepu       
Tunda huishia tumboni likianzia kwenye mbegu
Mama nimeshindwa sasa nawaachia walimwengu

Nakupigia simu hupokei, Nakutext ku-reply una-vex (vex)
Kwakuwa we ni mzuri unatafutwa na wengi hivyo unajiona keki, Mlemavu
Kutokujua kupenda si ujanja ni Ulemavu (yay yay yay yah)

Kwenye simu ulivyoni-save mi' fundi bomba
Ndo' nikajua inavyokata stimu kujikosha
Mioyo uliyoichukua ukaichezea na kuitupa
Utaenda mbali siku utarudi kuitafuta
Na hautaiona tena, aisee utaweweseka
Utapojua uzuri hauzuii kuzeeka
Utakufa hautaacha alama wala ngao
Kama urithi zaidi ya picha chafu kwenye mitandao
Namwonea huruma bwana'ko wa sasa si uongo
Huko aliko anahisi ameliokota dodo
Kumbe chizi uliyeshindikana milembe
Na kama unajiona mzuri sana jipende
Mchoyo mama una mtima wa aina gani
Utaacha lini hizo bima za wahisani
Moyo wako haujui kupenda asirani
Haujawahi hata kulala na picha kitandani
Haujawahi kuona watu wakighairi masomo
Wanazijua sheria, lakini bado wanavunja sababu ya kupenda
Wanakaidi maonyo
Haujui chochote zaidi ya hizo style za ngono
Rafiki yako Mage tumetoka kumzika
Wenye akili tumejifunza kwa huu msiba
Lakini wasio na haya, hawajui kuwa hakuna tuzo ya umalaya
Mwanaizaya pumzika
Ulinibeba ili uje kunitupa
Nilijiachia nimeumia sa' nimejifunza
Siwezi 'sema hautapata bwana kama mimi
Tupo wengi lakini utanikumbuka naamini

Nakupigia simu hupokei, Nakutext ku-reply una-vex (vex)
Kwakuwa we ni mzuri unatafutwa na wengi hivyo unajiona keki, Mlemavu
Kutokujua kupenda si ujanja ni Ulemavu (yay yay yay yah)
Nakupigia simu hupokei, Nakutext ku-reply una-vex (vex)
Kwakuwa we ni mzuri unatafutwa na wengi hivyo unajiona keki, Mlemavu
Kutokujua kupenda si ujanja ni Ulemavu (yay yay yay yah)

Watch Video

About Mlemavu

Album : Mlemavu (Single)
Release Year : 2022
Added By : Farida
Published : Jun 30 , 2022

More DIZASTA VINA Lyrics

DIZASTA VINA
DIZASTA VINA
DIZASTA VINA

Comments ( 0 )

No Comment yet



About AfrikaLyrics

Afrika Lyrics is the most diverse collection of African song lyrics and translations. Afrika Lyrics provides music lyrics from over 30 African countries and lyrics translations from over 10 African Languages into English and French

Follow Afrika Lyrics

© 2025, We Tell Africa Group Sarl