...

Fanani Lyrics by DIZASTA VINA


Talent and ability, can take you to the top of the mountain

Lakini, the moment you mess up with your character

Everything goes back to zero

Unaanguka chini kabisa

Natembea sehemu nyingi nakutana na

Watu wengi wananipa ushauri mwingi

Mwingi mwingi blah blah blah

Mbona hau-move hivi

Mbona sijui hau-force kingi

Mbona sijui hau-change hiki blah blah

Fanya collabo na flani na flani blah blah

Ule wimbo sijui ungemweka flani blah blah

Flani na flani sijui hawawezi fani, flani sijui hamjui flani

Flani sijui yuko kama flani blah blah

Mchumba anahisi nauza bangi

Anashangaa nimesoma sijatafuta kazi

Namwambia mistari yangu ni bidhaa

Nimelelewa vyema na sasa na sasa nailea hii mitaa

Mitaa inahisi nauza pakti

Nimechoka naunga waya naunga nyagi

Mwonekano nje hauonyeshi nina kisomo

Eti ubaya wa cover ndo' yaliyomo

Mama ana-wish nimwoe Tuntu

Anasema amesoma anamjua Mungu

Namwambia "Tuntu anawadharau ndugu"

"Na anaona mafanikio ni kupata bwana Mzungu"

Mama Tuntu anasema mi muhuni

Anahisi nipo ghetto nazienzi Kunguni

Haamini naheshimika kwa kuuenzi Utamaduni

Ana anahisi muziki dhambi kwahiyo siendi hata mbinguni

Hajui kuwa imani yake ni dau pana

La mchungaji, anahisi mi' mdhambi dharau sana

Nawa-overate watu nasahau kwamba

People with common sense mtaani are outnumbered

Mama anasema nabonga hanielewi

Nimezongwa siwezi kutoka na sihemi

Natembea na makaratasi utadhania Mkandarasi

Sina ganji utahisi nimerogwa na Washenzi

Namwambia "ujuzi power" nauhakiki

Nimenawa mpaka naenda sawa na Wahandisi

Wauguzi wanapagawa wakifika himaya hizi

Kuona Sina dawa utadhania mvuta kaya chizi

Mdogo wangu ana-doubt mi ni Star

Na anashangaa kwanini I don’t have a car

Washkaji daily wanataka tupige picha

Au short video Intro tukazitundike Insta

Chuki nikiwaambia niko busy

Hawaamini I have meetings to attend to

Wanahisi nawadanganya wakaulize

Kwani life is more than just Instagram and Facebook

Wanasema mi' kituko naruka luksi

Nishatengwa na milupo ila sikugeuka nuksi

Nilitishiwa hadi vifungo sikutupa ujuzi

Utotoni sikupewa maputo niliokota books

Sikupendwa na mazoba wakereketwa

Ni'shaibiwa na manyoka na ndio maana niko focus

Najua mikataba bogus inavyowateteresha

Ndo' maana huwezi kuona ninapelekeshwa

Naakutana na

Watu wengi wananipa ushauri mwingi

Mwingi mwingi blah blah blah

Mbona hau-move hivi

Mbona sijui hau-force kingi

Mbona sijui hau-change hiki blah blah

Fanya collabo na flani na flani blah blah

Ule wimbo sijui ungemweka flani blah blah

Flani na flani sijui hawawezi fani, flani sijui hamjui flani

Flani sijui yuko kama flani blah blah

Hauwezi ku-observe my position, my momentum

At the same time? that's cynical

I'm electron, I know how to move better, Kunidharau

Ni kuidharau Uncertainity principle

Naona wanaibuka Wanariadha

Wanafoka eti siongelei siasa

Sijabuma, najua mchezo, ni kwamba

Najua kukaa nyuma mbele masihara yakianza

Life is when things happen so, let it be

We learn how to behave from the same shit

Ninajua hizo struggle for revolution

And I knew it was time for change, so I change me

Masihara ni fashion ukihitaji ule

Hata vioo vya jamii vipo ndani mule

Wasanii wanatumia style yangu bure

Serikali hainitambui na ushairi wangu shule

Mitaani juu hela haishikiki

Nime-master mpaka school vyema hainishindi

Sina matatuu natembea kwa miguu wananishangaa

I'm getting too famous for this shit

I'm a big deal nasahau sahau bwana

Ila industry haiko real jau jau sana

Maudhui ni kitu wadau walikacha

Na maniga walisahau kuhusu culture

Kisa njaa kubwa

Mngekuwa wapi bila hiphop?

Mngeshika wapi hizo dough bila hiphop?

Mngekuwa wapi mapresenta wabovu

Makundi ya matozi na Hizi afternoon shows

Bila hiphop?

Ni vile ubishi nakazia

Hawaelewi kazi yangu maana dhiki imen'dandia

Mchumba n'nayembambia hasadiki nikimwambia

Mi' mwanamziki bado anahisi namtania

Anasema namletea msongo wa mawazo

Eti ooh! nimechoka na huo uongo wako

Ana hofu that we don't show off

Go out and hit a club like a normal couple

Kisa sija-fix my finances

She won’t fix her attitude

Anafungua fridge yangu na hajachangia kitu

Na anataka nimpeleke Summer Malibu

Namwambia I have real life sio sci-fi

Anahisi naishi honey boo boo lifestyle

Oohh she wanna dance in the car

40 degrees she wanna shake her ass in a Yatch

Natembea sehemu nyingi nakutana na watu wengi

Wananipa ushauri blah blah

Mbona haumove hivi sijui mbona hau force kingi

Mbona sijui hau.... blah blah blah

Blah blah blah

Blah blah

Ushauri mwingi blah blah

Man I'm outta here

Watch Video

About Fanani

Album : (Single)
Release Year : 2024
Copyright :
Added By : Farida
Published : Oct 23 , 2024

More DIZASTA VINA Lyrics

DIZASTA VINA
DIZASTA VINA
DIZASTA VINA

Comments ( 0 )

No Comment yet



About AfrikaLyrics

Afrika Lyrics is the most diverse collection of African song lyrics and translations. Afrika Lyrics provides music lyrics from over 30 African countries and lyrics translations from over 10 African Languages into English and French

Follow Afrika Lyrics

© 2025, We Tell Africa Group Sarl