Desh Desh Lyrics
Desh Desh Lyrics by LAVA LAVA
Mola kamuumba
Hana mfano weee
Mzuri w asura na roho
Na njema tabia iyaaa
Unyagoni kafundwa
Kwa makungwi somo weee
Mahaba kayajaza ndoo
Yananimwagikia iyaaa
Natamani nimtaje hata jina ila naficha naficha
Naifanya siri yangu
Kina fulani wale wakusigina mkaleta mapicha mapicha
Akatoroka ndege wangu
Si mrefu si mufupi (ah eh)
Si mweupe si mweusi (ah eh)
Rangi yake ni ya katikati
Kasima kwangu afurukuti (ah eh)
Kwengine anaogopa nuksi (ah eh)
Mi ni wake milele haniachi ndo maana
Nampenda mpenda (nani)
Kijana mmoja (nani)
Amenifika kwa roho makopakopa (kopa)
Nampenda mpenda (nani)
Kijana mmoja (nani)
Ila kumtaja ooh naogopa ogopa kwa jina namuhifadhi
Desh desh, desh desh
Msije kuninyakulia
Desh desh, desh desh
Kipenzi change jamani
Desh desh , desh desh
Mkaja kuniharibia
Desh desh, deeesh
Penzi likawa mashakani
Nananaa nna nna
Nananaa nna nna
Nananaa nna nna
Najua najua
Roho zinawauma
Hampendi kuona
Mwenzenu na nawiri
Najua mwenzenu najua
Mwakesha kujituma
Kutwa kwa masangoma
Yangu kuyatabiri
Mlosema nimeachika
Hainifiki mikosi
Mola ndo mpaji, nyongo mtazitapika
Mchomwe jua la utosi kesheni kunijani
Mwenzenu kila kukicha, kabla kupewa misosi
Masaji masaji tunavyowakasirisha
Yani hata tukiposti hataki nimtag
Enhe si mtu wamagazeti
Wala page za udaku ilo mkae mjue
Hataki taki eenhe
Mambo yake siri nyeti
Poleni washakunaku
Wala msijisumbue kumsachi sachi
Nampenda mpenda (nani)
Kijana mmoja (nani)
Amenifika kwa roho makopakopa (kopa)
Nampenda mpenda (nani)
Kijana mmoja (nani)
Ila kumtaja ooh naogopa ogopa kwa jina namuhifadhi
Desh desh, desh desh
Msije kuninyakulia
Desh desh, desh desh
Kipenzi change jamani
Desh desh , desh desh
Mkaja kuniharibia
Desh desh, deeesh
Penzi likawa mashakani
Nananaa nna nna
Nananaa nna nna
Nananaa nna nna
Watch Video
About Desh Desh
More LAVA LAVA Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
You May also Like
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2025, We Tell Africa Group Sarl