Mungu Wa Ibada Lyrics
Mungu Wa Ibada Lyrics by AMBWENE MWASONGWE
Wewe ni wengu, wewe ndiwe
Ulikuweko kabla ya mwanzo
Ulikuweko kabla ya miaka
Ndiwe uliweka mbingu za mbingu
Ulimweka kerubi
Akuabudu akafunika kiti
Kwa mbawa zake mlima wa moto
Wenye mawe ya moto akaabudu
Utukufu ukaonekana
Ila ukatazama moyo wa kerubi
Akajichuuza akajivuna
Uovu ukaone kana ndani yake
Akang’olewa akafukuzwa ibada ikaendelea
Maana wewe ni mungu mungu wa ibada
Ndipo ukaumba mtu kwa mfano wako, na sura yako
Ndipo ukamweka bustani ya edeni ukamtembelea
Ukaongea naye akakuabudu
Mungu wa ibada, wewe ni mungu
Mungu wa ibada
Wewe ni mungu chanzo cha vyote
Wewe ni bwana, injini ya vitu/vyote
Ndio maana wewe haulali
Ndio sababu, wewe husinzii
Siku ukilala itakuwa kasheshe
Maana vilivyolala vyote vitaamka
Vilivyo macho naamini vitalala
Itakuwa kasheshe na mtikisiko
Dude la baharini ndipo litaamka
Nani atalifunga joka lewithani ?
Bahari itakiuka sharia iliyowekewa nchi itakiuka
Amri uliyoipa vitu vyote vitakwenda
Bila sheria maana mweny sheria
Utakuwa umelala, asante maana hulali
Asante maana husinzii wewe ni injini
Ya kuendesha vitu vyote bwana unaweza
Bwana una nguvu
Wewe ni mungu wa ibada
Wewe ni bwana muumbaji
Sheria zote umeweka
Wewe ni bwana wa vitu vyote
Aaah aaaah aaah aaaah
Aaah aaaah aaah aaaah
Wewe ni mungu usiyeshindwa
Huhitaji jeshi kushinda vita
Huhitaji vingi kushibisha watu
Huhitaji mawe magumu kushinda
Daudi na mawe yake yale matano
Alitumia moja kwa jina la bwana
Chupa ya mafuta ilikuwa ndogo
Ila ilitosha kujaza mapipa
Watu wanne, tena wakoma na visigino vyao
Wakasikizisha vishindo, kwa jina la bwana
Jeshi likakimbia likaachia nyara
Huhitaji mapanga mengi, kuwapiga watu jeuri
Kwa malaika mmoja, wazaliwa wa kwanza walikufa
Farao alikoma, akamwambia musa nendeni
Kwawabudu Jehova, maana yeye peke yake ni mungu
Aaah wewe ni mungu, mungu wa ibada
Bwana tubaariki utulinde sote
Utupe roho wako, atuogeze kwa Yesu
Amen amen aameh
Kweli atukuzwe
Yesu ndiye bwana tu yeye utubariki
Wewe ni mungu wa ibada
Wewe ni bwana muumbaji
Sheria zote umeweka
Wewe ni bwana wa vitu vyote
Aaah aaaah aaah aaaah
Aaah aaaah aaah aaaah
Watch Video
About Mungu Wa Ibada
More AMBWENE MWASONGWE Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2024, We Tell Africa Group Sarl