Picha ya Pili Lyrics
Picha ya Pili Lyrics by AMBWENE MWASONGWE
Yahitaji macho ya moyo, kuona picha ya pili
Yahitaji sikio la ndani, kusikia sauti ya moyo
Nimeona chozi likitiririka, kwenye uso unaocheka
Nimesikia sauti ya kuugua, katikati ya kigelegele
Nimeona watu wakienda, kuwaona wahitaji
Ila wamebeba kamera uuuh! kuuonyesha ulimwengu
Yatima nao wajane, mbele ya kamera, hushukuru kwa kutabasamu
Ila wakibaki peke yao na Mungu hulia kwa kuugua
Sababu ya uyatima, sababu ya ujane, ni kama twadhalilishwa
Hawajui size ya kiatu hiki namna kinavyobana, Hawajui twaumia
Ni Yesu tu, Ni Yesu
Anayeletaga faraja ya moyo kwa aliyeumizwa na kuvunjwa vunjwa bila matangazo
(Wewe Yesu u mwema kwetu yooh!..)
Ni Yesu tu ,ni Yesu anayetoaga neno la faraja la moyo
Liwe hadharani au la sirini wala haliumizi
(Ni wewe ufanyaje kwa kutufikiria utu wetu)
Ni yesuuu tu ni Yesu
Anayetoaga Neno la Faraja Liwe hadharani au la sirini wala Haliumizi
Nilimwona mama analia, mtoto wake kawa teja
Anavuja mate mtaani, wenzake wanamcheka
Wanapiga picha naye wanafanya self wanapost wanacheka
Wanainjoi wanatafuta views hawajui maumivu ya mzazi
Kicha kwa mwenzako anachekesha sana, akiwa kwako anauma
Mlemavu kwa jirani anaburudisha, akiwa kwako anauma
Niliona wazazi wanalia eeeh! malezi yamewashinda
Wamejitahidi sana kusema, watoto hawasikii
Wanasikia mtaani wanasemwa vibaya, bado hawakati tamaa
Hata kama ni mwizi, hata kama malaya, ni mtoto wangu hakati tamaa
Ni Yesu tu, Ni Yesu
Asiyewatupa tusiowajali, tunaowasema tuliowachoka na kuwadharau (eeheee)
Ni Yesu tu Ni Yesu
Anayeletaga jibu la maswali kwa waliochoka
Wenye utata na waliokwama (eeeheee!)
Ni Yesu tu Ni Yesu
Anayeletaga jibu la maisha kwa waliochoka
Wenye maswali, na wenye utata. (Bwana nakuombaaa)
Naomba wakumbuke, tuliowachoka, tunaowasema
Tunaowadharau. Bwana warehemu ni watoto na utusamehe
Samehe makosa yetu samehe raha yetu
Tumefurahiii tukadhani tumefanya kwa ajili yao kumbe kwa ajili yetu
Samehe Bwana kuwatangaza wao bila kujali utu
Ni Yesuuuu Ni Yesuuu Ni Yesuuu oooh
Ni Yesuuuu Ni Yesuuu, Ni Yesuuuu, Ni Yesuuuu uuu
Watch Video
About Picha ya Pili
More AMBWENE MWASONGWE Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
You May also Like
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2024, We Tell Africa Group Sarl