Y PRINCE Mashujaa Wetu cover image

Mashujaa Wetu Lyrics

Mashujaa Wetu Lyrics by Y PRINCE


Aaah Tanzania, iye iye
Aaah Tanzania, iye iye
Aaah Tanzania(Selo beats)

Katika kila jambo
Unaloliona lapendeza
Jua kuna watu walioumia 
(Kwa ajili hilo) Aaah (Kwa ajili hilo) 

Katika kila jambo
Unaloliona lavutia
Jua kuna watu waliotaabikia 
(Kwa ajili hilo) Aaah (Kwa ajili hilo) 

Ni kweli Tanzania kuna amani ya kutosha
Hilo tunajivunia
Yatupasa tuliombee jeshi letu la taifa
Mola alotujalia 

Wanapambana kwa ajili yetu oooh
Ili tuwe salama salama 
Wanahangaika usiku na mchana oooh
Miili yao wametoa sadaka oooh

Wanalala kwenye vumbi na matope
Ili sisi tulale vitandani mwetu
Tunatembelea magari ya dhamani sana
Wanatembelea vifaru na malori

Asubuhi 
Unaamshwa na alamu ya simu yako
Wao wanaamshwa 
Kwa milio ya mabomu na risasi

Wanatoa sadaka yao leo 
Kwa manufaa ya kesho yako
Wameyatoa sadaka ya maisha yao
Ili kutetea maisha yako

Twaiombea nchi yetu(Ooh Tanzania)
Nchi yetu(Ooh Tanzania)
Twaiombea jeshi letu(Mashujaa wetu)
Jeshi letu(Mashujaa wetu)

Twaiombea nchi yetu(Ooh Tanzania)
Nchi yetu(Ooh Tanzania)
Twaiombea jeshi letu(Mashujaa wetu)
Jeshi letu(Mashujaa wetu)

Unavaa mkanja mzuri kiuoni mwako eeh
Wanavaa mikanja ya risasi..ii..ii...ii 
Unakula chakula ukipendacho, kile ukitamanicho
Wanakula wadudu na matunda porini(porini)

Tunavaa kofia maridadi 
Na nzuri zenye kupendeza
Wanavaa kofia ngumu 
Na nzito tena za chuma

Sijutii kuzaliwa Tanzania
(Aah...)
Najivunia mimi kuwa Tanzania 
(Aah...)

Wanapambana kwa ajili yetu oooh
Ili tuwe salama salama 
Wanahangaika usiku na mchana oooh
Miili yao wametoa sadaka oooh

Asubuhi 
Unaamshwa na alamu ya simu yako
Wao wanaamshwa 
Kwa milio ya mabomu na risasi

Wanatoa sadaka yao leo 
Kwa manufaa ya kesho yako
Wameyatoa sadaka ya maisha yao
Ili kutetea maisha yako

Twaiombea nchi yetu(Ooh Tanzania)
Nchi yetu(Ooh Tanzania)
Twaiombea jeshi letu(Mashujaa wetu)
Jeshi letu(Mashujaa wetu)

Twaiombea nchi yetu(Ooh Tanzania)
Nchi yetu(Ooh Tanzania)
Twaiombea jeshi letu(Mashujaa wetu)
Jeshi letu(Mashujaa wetu)

Twaiombea nchi yetu(Ooh Tanzania)
Nchi yetu(Ooh Tanzania)
Twaiombea jeshi letu(Mashujaa wetu)
Jeshi letu(Mashujaa wetu)

Twaiombea nchi yetu(Ooh Tanzania)
Nchi yetu(Ooh Tanzania)
Twaiombea jeshi letu(Mashujaa wetu)
Jeshi letu(Mashujaa wetu)

Watch Video

About Mashujaa Wetu

Album : Mashujaa Wetu (Single)
Release Year : 2019
Copyright : (c) 2019
Added By : Huntyr Kelx
Published : Jul 20 , 2019

More Y PRINCE Lyrics

Y PRINCE
Y PRINCE
Y PRINCE

Comments ( 0 )

No Comment yetAbout AfrikaLyrics

Afrika Lyrics is the most diverse collection of African song lyrics and translations. Afrika Lyrics provides music lyrics from over 30 African countries and lyrics translations from over 10 African Languages into English and French

Follow Afrika Lyrics

© 2024, We Tell Africa Group Sarl