
Usichelewe Lyrics
...
Usichelewe Lyrics by WALTER CHILAMBO
Aaaah
Walter tenaaa
Mungu wangu
naomba niongee na wewe
Hata kidogo
Nasikia uchungu ndani ya Moyo
Mambo yamekuwa mazito
Na siwezi peke yangu
Naona maumivu ndani ya moyo
Na umesema walipo wawili wewe upo
Najiuliza nikiwa peke yangu je we upo?
Ni kweli na imani
Lakini kuna muda nachoka
Na si kwamba sikuamini
Nakuamini sanaa
Nimeomba,nimefunga na nimetoa sadaka
Ila mambo yanayumba,fanya hima uje haraka
Basi uniambie mi (Ni wapi nakosea)
Baba uniambie mi (Niwapi nakosea)
Yesu uniambie eehh (Niwapi nakosea)
Baba uniambie Mi niwapi nakosea nakuomba
usichelewe...( nachoka, nachoka )
usichelewe...( tazama moyo umechoka )
usichelewe...( nitangoja, ntangoja )
usichelewe...( Mi mwanao bado ntangoja )
Wenzangu wana marafiki
Wa kuwaambia shida zao
Na mimi we ndio wangu RAFIKI
Ninakuambia haja zangu
Siulisema
Utanibariki mjini na mashambani
Siulisema
Niingiapo na nitokapo nitabarikiwa
Siulisema
Fedha na dhahabu vyote ni mali yako
Siulisema
Nikiomba utanipa zaidi ya niombavyo
Nimeomba,nimefunga na nimetoa sadaka
Ila mambo yanayumba,fanya hima uje haraka
Basi uniambie mi (Ni wapi nakosea)
Baba uniambie mi (Niwapi nakosea)
Yesu uniambie eehh (Niwapi nakosea)
Baba uniambie Mi niwapi nakosea nakuomba
usichelewe...( nachoka,nachoka )
usichelewe...( tazama moyo umechoka )
usichelewe...( nitangoja ,ntangoja )
usichelewe...( Mi mwanao bado ntangoja )
Watch Video
About Usichelewe
More WALTER CHILAMBO Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
You May also Like
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2025, We Tell Africa Group Sarl