RUBY Ntade cover image

Ntade Lyrics

Ntade Lyrics by RUBY


Ile mito milima tuliopita uliiona
Nikavumilia nika ng'ang'ana si unaona
Kuna vijidada vinadanga utaona
Vikijipitisha vinatingisha utaona

Wambieee... siongezi neno nishaweka nukta
Wajue... Nilitulia sikukurupuka
Wambie eeehe umenibana sitofurukuta
Mie nipeleke vyovyote mwendo wa guta

[CHORUS]
Hata uuze karanga (sawa, sawa)
Nimeridhia kidogo tutachanga (sawa, sawa)
Hey! Wanasema umenipiga manyanga (sawa, sawa)
Niroge niue nimefundwa na nyakanga(sawa, sawa)

Nikumbate kama mtoto
(Ntadeka ntade... Ntadeka ntade)
Tena unipe penzi moto moto
(Ntadeka ntade... Ntadeka ntade)
Babaa wewe (Ntadeka ntade)
Baba ba baba....

Naheshimu maamuzi maana
Nimempenda mwenyewe
Nishayavulia nguo bwana
Acha nioge
Ananikuna panapo kunika nikiwashwa
Ananishona palipo chanika sitomwacha
Ila unajuaga mimi mwenzako
Nakupenda napenda kweli kweli
Tena baby mwenzako mimi
Endapo ukinitenda utantenda kweli kweli
[CHORUS]
Hata uuze karanga (sawa, sawa)
Nimeridhia kidogo tutachanga (sawa, sawa)
Hey! Wanasema umenipiga manyanga (sawa, sawa)
Niroge niue nimefundwa na nyakanga(sawa, sawa)

Nikumbate kama mtoto
(Ntadeka ntade... Ntadeka ntade)
Tena unipe penzi moto moto
(Ntadeka ntade... Ntadeka ntade)
Babaa wewe (Ntadeka ntade)
Baba ba baba....
(Ntadeka ntade)
Ntadeka …(Ntadeka ntade)
Ntadeka, ntadeka, ntadeka we
(Ntadeka ntade)
Uuhhh (Ntadeka ntade)
(Ntadeka ntade)

 

Watch Video

About Ntade

Album : Ntade (Single)
Release Year : 2018
Added By : Afrika Lyrics
Published : Sep 18 , 2018

More RUBY Lyrics

RUBY
RUBY
RUBY

Comments ( 0 )

No Comment yetAbout AfrikaLyrics

Afrika Lyrics is the most diverse collection of African song lyrics and translations. Afrika Lyrics provides music lyrics from over 30 African countries and lyrics translations from over 10 African Languages into English and French

Follow Afrika Lyrics

© 2024, We Tell Africa Group Sarl