Kisanga Freestyle (TwoFiveVibes 5) Lyrics
Kisanga Freestyle (TwoFiveVibes 5) Lyrics by RAPCHA
(Last King of 90's baby)
Youngstar naitwa Rapcha
Mchizi toka Shaytown
Nina bar nyingi ka Sinza
Wanangu naitwa nani?
Jana njaa imenipiga nusu kuniua
Sema getto hamna Friji ningepata hata Ka juice unajua
Baisa Aliacha buku mezani
Nikasmile kisha nkajivuta kwa muha
Nipate japo hata vitumbua
Afu nkakumbuka juzi kuna deal niliipata
Nikamwambia mwana leo ntatua
Hapa ndo nna buku tu hesabu ishazingua
Sasa niifanye nauli ama msosi, bwana dar kuna jua!
Nkaona okay isiwe tabu jero acha niupe
Mwili nguvu kwanza hayo mengine mbele ntajua
Nkavuta trouser nkavaa
Ile shati ambayo siipendi Ndio safi zile nzuri zote sijafua
Nkaishi nalo tu afu nkachafua
Naingia zangu kwenye gari mlangoni konda ananisanua
Kuna siti moja empty ilobakia ipo pale kati
Sema mwana una bahati unajua
Nkamwelewa pale macho yalipotua kwenye siti iliobakia
Ah we leo mtanitambua
Huyo demu alivyo mzuri jua
Hata dem mwenzie angemuona angetamani kuwa mwanaume unajua
Dem mzuri kama huyuu kwenye daladala anatafuta nini
Inaweza ikawa mitego unajua
Ah bwana ee mbona mi mwenyewe ni msanii nashangaa mjini
Hela ya kula tu inaizingua
Nkampa mambo, Dada mbona kinyonge hauna bando
Haifai ukiwa hivyo we mrembo unajua
Akajibu poa, uchovu unazingua tu
Kaka afu umesahau funga zipu ya suruali unajua
Eh hilo jicho nlivyotumbua
Nikaifunga nikakaa kinyonge kiherehere kishaniumbua!
Sa nkawaza, huyu mtoto dafu ntafua
Nijiangushe ndani ya kumi na nane au nabutua
Afu kwanza hela yenyewe sina unajua
Mrembo kama huyu napata wapi nguvu ya kumsumbua
Ah sista we mkarimu sana nmegundua
Tujuane majina ukute sie ni ndugu hatujajua
Naitwa "Perry", perry perpetua
Ushaniperpertuate mpaka hapa we hujajua
Nkaanza kujipokelesha ma simu
Akatupa jicho kwenye simu akaona jina analolijua
Huyo ni FA? Khaa! Kumbe nani ukajua
Ni bro angu ukinijua mimi umemjua
Nkajipokelesha simu nyingine
Kasoma jina Vanessa mdee, kaka huyo nae unamjua
Nkambia hiii, Dada sio eti namjua tunajuana
We ishi na mimi mbona hata Rotimi atakujua
Naitwa Rapcha mtata
Mzee wa kufanya wanafyata
Huko kote wananipata swadakta
Nakulaga bata masaki osterbay na tabata
Ukinikuta na hela utanitaka!
Kumbe we star ndo najua
Ah tatizo upo slow sana dada umechelewa kunijua
Nkachukua point tatu mjuba
Nishapitiliza nlipokua nashukia vituo kama Tisa unaambiwa
Nkampa simu aandike namba akachukua
Hajaisave ikazima chaji huu si ndo uchawi unajua
Akanambia hapa mi ndo nashukia
Na baba yupo kituoni ndo amekuja kunichukua
Macho yalinitoka
Akashuka anatingisha hata nguvu ya kumtamani nilikosa unaambiwa
Jero langu nishalipia ntafikaje
Nlipokua naenda kwenye deal nishachelewa!
Ile natupa macho pale mtoto aliposhukia
Naona sura ya mzee kama na mjua
Afu macho yakakutana akatabasamu kwa bashasha
Nkaona nshuke huenda akanisave unajua
Sasa yule mzee alipo nkaanza
Kusogea yule manzi nae akawa anasogea
Mzee akafunguka Perry naona umeongozana
Na binamu yako sikujua kama unamjua
Nguvu ziliniisha unajua
Ah mzee shkamoo, marahaba eh Rapcha umekua
Juzi tu ulikua Mtoto nlikupeleka jando
Wakakukata govi saivi ushaanza masebene itakua
Ah kumbe huyo dem ni mtoto wa ba mdogo
Bwana usimvae mtu usiemjua
Nikimcheki tunatazamana tunacheka
Chinichini najiuliza vipi ningebutua
Basi ndo ivo mzee akanipa nauli ya kurudia
Na hii ndo story nzima ilivyokua
Watch Video
About Kisanga Freestyle (TwoFiveVibes 5)
More RAPCHA Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
You May also Like
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2025, We Tell Africa Group Sarl