Darasa Huru Lyrics
Darasa Huru Lyrics by NACHA
Asalaam Aleikum
Kwa jina la baba la mwana
Na la roho mtakatifu
Karibu kwenye darasa huru
Mwandishi wako ni Nacha
Kiingilio ni macho yako tu na masikio tu
Kisha maadili unapata
Mnyasubi ndani ya mbanyu
Mziki wako Nacha ni shule
Mafans wengi ndo wanavyoniambia
Na nilivyompenda sifa huwa nawajibu
Hii ni zaidi ya three sisters
One husband ni ya walioniambia
Karibu kwenye darasa huru
Utakula kwa jasho
Kwa hivyo kupambana inakulazimu
Mi mwenzako sina hamu
Nikikumbuka nilivyopoteza muda kutembea
Umbali mrefu toka Nyasubi mpaka Nyanga B primary
Kusoma maarifa ya jamii na sayansi kimu
Elimu ni ufunguo wa maisha wow
So waliosoma na hawana kazi mpaka sasa
Funguo zao zilipotea mnamaanisha au?
Anyways nisikilize kwa makini
Tuendelee kupata darasa huru
So hata kipindi si ni watoto wadogo
Wao wamelala asubuhi wakingoja breakfast
Si tulibeba jembe, tukiwa peku kwenye mvua tukilima
Tulikomazwa kabla ya muda maana huwezi kula ukiwa mzembe
Eeh ndo maisha yalivyo wao walilala pazuri
Si ilikuwa taabu mpaka pa kukaa
Tukimsaidia Bi mkubwa kupika vitumbua kisha tuwai shule
Wao waliwaambia mama zao "Hey mum can I use your car?"
Karibu kwenye darasa huru
Jamani ligi yetu itasimama kupisha maonyesho saba saba
Haha hii ni hatari ni sawa na mtoto kuzaliwa
Na kujiona ni baba mbele ya baba
Alafu tunataka tuwe na ushindani bora wa soccer kamatika
Yaani kwenye rank za Cafu
Tuwe juu mbele ya al ah-hari
Raja na waidad Casablanca,
Zamalek, Enyimba mamelord
Asante kotoko na Ace Vita
Hizi ni hadithi za Abinuwasi
Twendelee kupata darasa huru
Tukitaka kuwa bora ni lazma kwenye sekta nyeti
Tuweke watu wenye weledi
Otherwise mafanikio na ustawi wa soccer letu
Tutayaskia kwenye stori za Juma na Uledi
Mafans wanahoji Nacha mbona kila ngoma ukitoa inatrend
Alafu heshima kama hupewi
Na majibu nililetwa kwa ajili ya watu wenye akili ya ziada
Ndio maana wenye akili ya kawaida hawanielewi
Zamani tulikuwa tukitoka shule ni tuition
Au homework kisha kazi
Sa hivi wakitoka shule ni remote au kushika pad
True difinition ya talent ngumu kupata zama hizi
Mkono wa kushoto nitamchora Ngwear
Mkono wa kulia nitamchora kingz la zizi
Tatizo ni kwamba hatuelewi tunakariri
Yaani hatuna utofauti na wanao amini
Kumwabudu Mungu ni ijumaa na jumapili
Utakwenda peke yako kaburini ukakae
Ndugu zako nyuma wakilia
So wake-up brothers and sisters
Swali kabla hujasaliwa endelea kupata darasa huru
Wakiniuliza Nacha nani ni kocha bora kwako wa dunia
Kati ya Carlo Ancelot, Zinadine Zidane, Mourinho
Eugene Clop na Pepe Gardiola
Mi mzalendo kwa iyo nitawajibu
Juma Mgunda, Mark Meksime, Charles Bonface Mukwasa
Na Suleiman Matora
Superwoman ulipoumia alikuhudumia
Alihakikisha halali mpaka we ulale
Alikutibu ulipoumia, alikaa na njaa ili we ushibe
Na alikufundisha maadili ya heshima
Vya watu usiibe
Familia bora inajengwa na mwanamke
So big up kwa wanawake wote duniani
Umevijulia ukubwani wacha kuparamia
Unamtumia nauli mpenzi uliyekutana naye Facebook
Mwisho wa siku unalia
Unachomiliki ni group la Whatsapp tu na unaturingia
Kwenye magroup ya discussion we ulikuwa unasinzia
Okey tujuze, uko group gani? Amphibian au mamalia
So take care anaweza kuwa chanzo
Cha kufanikiwa au kutofanikiwa anaitwa rafiki
Na mnachokosea ni kuamini sita ni sita tu
Hata igeuzwe vipi kaa kwa kutulia
Endelea kupata darasa huru
Utazeeka nyumbani wewe kwa kukataa mume
Kujaza vipodozi kwenye dressing table kujipodoa
Hizo high heels Brazilian hair
Kope na kucha zina muda wake
Dhamani ya mwanamke ni ndoa
Na mi sio mbaguzi
Ila huwa nakuwa mbaguzi inapobidi
Na sioni ka nakosa
Ronaldo na Messi ni bora
Ila kwangu bora ni Lunya Mila
Tariba West, Samuel Etoo, Victor Wanyama
Mbwana Ali Samatta, Nwanko Kanu
Ali Mayai Tembele, Didier Drogba
Elhaji Diof na JJ Okocha
Kuuficha uhalisia usikuumbue
Ni sawa na kuficha ujinga
Kwa hiyo endeleeni kukazana kumeza P2
Kwa lengo la kuzuia mimba
Si hatuhitaji favour nyingi ndo tufanikiwe
Au sio sisi?
Si tunahitaji fedha kidogo tu ili tuzalishe
Ufanikiwe na wengine wafanikiwe kupitia sisi
Tuko sawa tuko sambamba mpaka hapa
Okay twendelee kupata darasa huru
Si hatukuzaliwa kwenye fedha nyingi
So ilibidi kuzitafuta bila kuwaza
Tulizaliwa kwenye familia za kujishikiza
Tusife njaa sio kula na kusaza
Na ninachomwomba Mungu anitimizie kabla sijafa
Sio kuweka baa heshima na akina Tina
Bali anipe nguvu na uwezo wa kufika
Jerusalem, Macca na Madina
Mi sio mkamilifu ndio maana nikikosea huwa natubu
Nilijifunza kujitegemea peke yangu
Bila kumtegemea jamaa rafiki wala ndugu
Huwa nasikitika sana kuona vijana wa sasa
Wakitembea wamevaa uchi, ooh sorry wamevaa Gucci
Ni ujinga kudhamini kuvaa kuliko mambo msingi
Huo ni uzushi, punguzeni kiherehere
Maana ndani kundi lenu kuna msaliti
Alafu mnaweka kikao cha nani atamfunga paka kengele
Mi sikuwahi kubebwa
Ndio maana wanaobebwa huwa nawabeza
Na mkitaka kuwashindanisha
Wao na Nacha nani anapendwa mitaani
Hakikisheni mmebeba jeneza
Aku mi wala sina wasi
Nyuma mna nyuni alafu cotton hio ndani
Golini Kaseja, mnakufa tatu bila
No retreat no surrender
Yaani kufa ndo kufeli
Maana si bado mnangoja kuona zama hizi
Kuku akipanda baskeli
Kemea mapepo hii ngoma inauma kama mbu
Angatao wakati wa prep
Dogo kazana shule
Haki ya elimu hii isiyo na visheti
Usichokijua ni kwamba yule role model wako
Kwenye social network ana fake
Napokosea na tunakaa kimya
Sio kwamba hatuna mdomo msidhani
Maana kwa jinsi tunavyozidi kupromote ujinga
Ndo tunavyozidi kujitukanisha nchi jirani
Mazuzu bado wanashangaa kwa nini sindano inazama
Na meli inaelea
Usijiptape sana ndugu safari ingali bado inaendelea
Nataka niache pengo na alama siku nikifa
Kama mzee wangu Julius, Mandela, Mugabe
Walazwe pema nguli wa Africa
Wakibomoka huwa nawajenga
Aluta continua bado hatujafika
Lakini bado pia hatujaacha kwenda
Mi nimeshakuwa ndio maana sivuti chochote
Zaidi ya uradi kwa tasbii
Yes bado hamjajua kutofautisha ipi ni siasa
Na ipi ni ukweli sahihi
Cha kushangaza ni kwamba mnatumia nguvu nyingi
Kupromote uongo mbele ya ukweli
Watu wanajua mbivu na mbichi kwa hio uongo kwaheri
Nawashangaa nimekuwa na wao na wao ni matajiri
Wananicheka nilipoteza muda mwingi
Kujifunza hesabu za kipeuo cha pili
Kisichokuwa na dili
Ni kwamba tunachelewa kufanikiwa
Sababu hii vita unaipigana peke yako
Mwenzako anaipigana nyuma akiwa na backup
Ya kaka, dada, mama, shangazi na uncle
Dah hamfanyi kazi na mnangoja mafanikio
Haki ya nani okey endeleeni kusubiri pera
Chini ya mpapai huku mkitafuta mchawi nani
Ulichokosea ni kwamba ulitegemea
Kuvuna kipindi mkulima kala mbegu
Hapo ndo ulipokosea so please
Jitahidi sana usiwaangushe wanaokutegemea
I go by the name N.A.C.H.A
Aka Nacha Nyasubi ndani ya mbanyu
Watch Video
About Darasa Huru
More NACHA Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
You May also Like
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2025, We Tell Africa Group Sarl