Sina Neno Lyrics
Sina Neno Lyrics by JUX
Naona wameremeta ngozi imenawiri
Una furaha now
Kitanda hakina siri
Zao la tendo una kitumbo wow!
Mnapendeza na pendo liko kasi kasi
Mkipostiana Instagram Status
Tushafunika kurasa mambo ya zamani
Yalishapita
Maisha mengine sasa
Kuwa na amani hakuna vita
Sikuchukii nakuombea
Maisha mema ya furaha
Mungu aonyeshe njia
Silii mimi nimezoea
Ila nina furaha kuiona familia
Niko salama, mimi sina neno (Aaah)
Utaitwa mama mtoto mpe upendo (Aaah)
Niko salama, mimi sina neno (Aaah)
Utaitwa mama mtoto mpe upendo
Najua unayo furaha kwa zawadi uliyopata
Tena ulivyo shujaa mtoto mama amepata
Na nyie msijegombana mtoto akapata kash kash
Vizuri kuvumiliana matatizo mka-discuss
Tushafunika kurasa mambo ya zamani
Yalishapita
Maisha mengine sasa
Kuwa na amani hakuna vita
Sikuchukii nakuombea
Maisha mema ya furaha
Mungu aonyeshe njia
Silii mimi nimezoea
Ila nina furaha kuiona familia
Niko salama, mimi sina neno (Aaah)
Utaitwa mama mtoto mpe upendo (Aaah)
Niko salama ...aaah aah (Aaah)
Utaitwa mama mtoto mpe upendo
Watch Video
About Sina Neno
More JUX Lyrics
Comments ( 0 )
No Comment yet
Get Afrika Lyrics Mobile App
About AfrikaLyrics
Follow Afrika Lyrics
© 2024, We Tell Africa Group Sarl