Harusi Lyrics by JOVIAL

Harusi ni ya Mola eh, hee
Leo nalikamilisha aah
Ubachela kwaheri, kwaheri
Nabadilisha maisha, aah

Umenipa maruani, hata siamini
Umenikubali
Umejua kuniheshimisha mbele ya waumini
Umefunua umwari

Mashallah, mejaliwa uzuri 
Wa sura na tabia, aah tena
Hee wallah, tulizungushe bakuli
Wenye nacho kuchangia, aah aah

Leo naoa, naoa
Naoa mie 
Leo naoa, naoa
Naoa mie 

(Mmmm mmmh mmh)

Machozi ya furaha yananitiririka
Yaani kama ni kama mazihara, naolewa mie 
Zichepuke balaa, umeniona mimi mbele ya wengi
Umenipa ushujaa, nitake nini mie?

Watu wamependeza, ona wanavyocheza 
Baba umeniweza, ng'ang'ania
Mashallaah hujajaliwa kiburi
Usemacho wasikia, aah ah

Hee wallah, tulizungushe bakuli
Wenye nacho kuchangia, aah aah

Leo naolewa, naolewa
Naolewa mie 
Leo naolewa, naolewa
Naolewa mie 

Wale wa ubwabwa 
Wamekamata matonge matonge
Leta champagne
Tugoganishe vikombe vikombe

Ah kule wa kucheza
Wanazungusha miuno si --
Leo ni kushiba 
Tutoke ndani vibonge vibonge

Music Video
About this Song
Album : Harusi ,
Release Year : 2020
Copyright : (c) 2020
Added By: Huntyr Kelx
Published: Apr 25 , 2020
More Lyrics By JOVIAL
Comments ( 0 )
No Comment yet