...

Unanifaa Lyrics by IYANII


Nataka kuwa na wewe

Siku zote za maisha yangu, malaika

Kwa maisha yangu

Ni wewe daima

Nakupenda sio siri

Na unajuwa shahidi mungu wangu

Fundi wa raha zangu

Ni wewe daima

Harusi tufanye na wewe

Uhame ukuje tuishi kwangu

Watoto wafanane na wewe

Lakini macho wachukue zangu

Tuishi tuzeeke na wewe

Nikifa uzikwe kando yangu

Kwa macho yangu

Ni wewe unanifaa

Ntakupenda mpaka siku watanizika

Nauliza umekuwa wapi

We mpenzi wa roho yangu

Umekuwa wapi

We mzazi wa watoto wangu

Umekuwa wapi

Wewe mboni ya macho yangu

Kwa macho yangu

Ni wewe unanifaa

Ntakupenda mpaka siku watanizika

Bahari ya mapenzi

Tuogelee tukiwa wawili baby

Naahidi kukuenzi siku zangu zote

Za uhai mpenzi

Nina kosa usingizi bila wewe

Mapenzi yangu kwako

Ni ya milele ningependa

Tuishi wawili kwa dunia

Kwa mawingu me na we

Mpenzi twa pepea

Hili ndio dua langu

Kwa mwenyezi nakuombea

Kwa macho yangu

Ni wewe unanifaa

Ntakupenda mpaka siku watanizika

Nauliza umekuwa wapi

We mpenzi wa roho yangu

Umekuwa wapi

We mzazi wa watoto wangu

Umekuwa wapi

Wewe mboni ya macho yangu

Kwa macho yangu

Ni wewe unanifaa

Ntakupenda mpaka siku watanizika

Watch Video

About Unanifaa

Album : (Single)
Release Year : 2025
Copyright :
Added By : Farida
Published : Apr 23 , 2025

More IYANII Lyrics

Comments ( 0 )

No Comment yet



About AfrikaLyrics

Afrika Lyrics is the most diverse collection of African song lyrics and translations. Afrika Lyrics provides music lyrics from over 30 African countries and lyrics translations from over 10 African Languages into English and French

Follow Afrika Lyrics

© 2025, We Tell Africa Group Sarl