STAMINA Nitakukumbuka  cover image

Paroles de Nitakukumbuka

Paroles de Nitakukumbuka Par STAMINA

Ule msemo wako kuwa uone kweli mama
Nimeyaona kweli dunia hadaa
Ili uyashinde yanahitaji ushujaa
Nami mwana bado napambana mama

Nitakukumbuka daima, nitakukumbuka kila siku
Nitakukumbuka daima, nitakukumbuka kila siku
Nitakukumbuka daima, nitakukumbuka kila siku
Nitakukumbuka daima, nitakukumbuka kila siku

Mama mama mama nakuita mara tatu
Ningepewa uwezo ungefufuka toka wafu
Nachokumbuka baba alikupenda pengine
Maana tangu uondoke naye hajaoa mke mwingine

Nimepitia vingi nimekuwa star mami
Na nchi imeandika historia maana presida ni woman
Nakumbuka ulikuwa na ndoto ya kuwa rais wa nchi hii
Namchukia Izraeli kwa kukatisha ndoto hii

Mama alafu ulikujua kuwa una ndugu wanafiki
Hawakuja kukuzika na hawakusema wako wapi
Nilimwona mjomba na mama wadogo kadhaa
Ila shosti wako bwana hakuja alikesha baa

Uliniambia nioe unakumbuka sindio
Nilioa mama tena kwa shangwe na mapambio
Yalitokea mazito mazito yenye vilio
Ila sa ivi nina mkwe mwingine 
Na mjukuu anaitwa Lio

Ule msemo wako kuwa uone kweli mama
Nimeyaona kweli dunia hadaa
Ili uyashinde yanahitaji ushujaa
Nami mwana bado napambana mama

Nitakukumbuka daima, nitakukumbuka kila siku
Nitakukumbuka daima, nitakukumbuka kila siku
Nitakukumbuka daima, nitakukumbuka kila siku
Nitakukumbuka daima, nitakukumbuka kila siku

Ndoto ya kambumbu kusakata iyo kwangu ilikuwa dili
Sikupata nachotaka nimepata nachostahili
Hii dunia ya wajuaji yenye mengi makelele
Ambayo ukipanda mnazi eti ukae siti ya mbele

Nimekumbuka kipindi nikilia unaninyonyesha
Nikichafuka fasta mama unaniogesha
Vipande vya vitenge na zile nepi za kuegesha
Lile ni vazi la afya nashukuru mama ulinivesha

Mama I cry for you, I love you
Hata kama kufa I will die for you
Sijapata kitu mpaka leo nipo choka
Mi kivuli kilichopinda kwenye mti ulonyooka

Wanasema marehemu anakuwa karibu na Mungu
Mwambie basi anipe hela nahitaji ilo fungu
Kuna mama mwenye nyumba na mama ambaye ni mchumba
Ila wote mama wadogo mkubwa mama alin....

Ule msemo wako kuwa uone kweli mama
Nimeyaona kweli dunia hadaa
Ili uyashinde yanahitaji ushujaa
Nami mwana bado napambana mama

Nitakukumbuka daima, nitakukumbuka kila siku
Nitakukumbuka daima, nitakukumbuka kila siku
Nitakukumbuka daima, nitakukumbuka kila siku
Nitakukumbuka daima, nitakukumbuka kila siku

Ecouter

A Propos de "Nitakukumbuka "

Album : Paradiso (Album)
Année de Sortie : 2021
Copyright : (c) 2021
Ajouté par : Huntyr Kelx
Published : Dec 17 , 2021

Plus de Lyrics de STAMINA

STAMINA
STAMINA
STAMINA
STAMINA

Commentaires ( 0 )

Aucun commentaire pour l'instant

A propos de AfrikaLyrics

Afrika Lyrics est la plus large collection de paroles de chansons et de traductions d’Afrique. Afrika Lyrics fournit les paroles des musiques de plus de 30 pays africains et des traductions de lyrics de plus de 10 langues africaines en français et en anglais.

Suivre Afrika Lyrics

© 2024, We Tell Africa Group Sarl