Paroles de Asiwaze
Paroles de Asiwaze Par STAMINA
Stamina ft Atan - Asiwaze lyrics
(Kiri! Bear)
Iye iye iye iye iyeee iyee
Iye iye iye iye iyeee iyee
Aaah unaposkia neno ndoa(Ndoa)ujue noma
Kabla kuongea chochote
Naomba kwanza kusonya(Msschew...)
Sijali nishauri nani aisee ok twende
Aliyenifundisha mapenzi
Hakuniambia kuhusu kuoa
Alinionyesha staili za tendo
Ila sio maisha ya ndoa
Aliyesema ndoa ndoano
Hivi huyu mjinga ni nani?
Kafanya nivue samaki
Kwenye bahari yenye tsunami
Nikiziona picha za harusi
Najiskia vibaya
Namuonea huruma padri
Pamoja na waimba choir
Yale mafunzo ya katekista
Eti yamepotea mazima
Sadaka misa ya ndoa
Bora mngewapa watoto yatima
Pole wasimamizi wa ndoa
Kwa ujinga mliosimamia
Mngesimamia ukucha
Mngekuza hata familia
Kama ni pete
Nisharudisha kwa sonara
Tayari nishavuta mpunga
Nimerudisha nusu hasara
Kabla kuingia ndoani
Anakuwa kondoo usiyemjua
Ila ukimweka ndani
Nyani anakuachia mabua
Marafiki, mashemeji
Ndio wanafiki nakuambia
Wanaweza kufanya ulewe
Bila hata kukupa bia
Sasa ile suti(Ilifanya ya nini? )
Na mchango(Nilichangisha ya nini?)
Na wale ndugu(Niliwaita wa nini?)
Na kile kiapo(Niliapa kwa nini?)
Naubembeleza upepo
Usizime kibatari(Iye iye iye)
Kichwani mwangu hayupo
Moyoni niko shwari(Iye iye iye)
Ona hajaacha pengo mwambie, asiwaze
Huko aliko atulie, asiwaze
Kama amepoteza lengo mwambie, asiwaze
Huko aliko atulie, asiwaze
Mwambieni yule dogo aliyeichezea club ya Simba
Kutembea na mke wangu asijione kama ameshinda
Mi samaki, mapenzi yangu yana chombo
Kaka yake nishakula so ruksa kutoa vyombo
Hata posa nililotoa mwambieni aingize vikoba
Ila atakaye muoa ampe mtaji wa bodaboda
Ama kweli hii dunia ina mambo mengi
Na ndoa ni kama boti haiwezi kupaki stendi
Hichi cheti cha ndoa nimebaki nacho kwa nini?
Siwezi kuombea kazi hakina mchongo apa mjini
Hata Biblia imeandika wanawake tuishi nao kwa akili
Kwao sikumficha kitu ulimpa hadi sehemu za siri
Akiskia nimekufa mwambieni asilie sana
Aite rafiki wafurahi wachome nyama
Nitazikwa na ndugu, rafiki na mafans kibao
Mkimuona msibane nitafufuka nimzabe vibao
Unaweza kumpakia mkongo mkeo na usimfikishe
Alafu anayempakia mkorogo ndio akamfanya amridhishe
Ndoa ndoana anayebisha aniulize mimi
Nishawahi kuwa na mahusiano
Ambayo sijui yanahusiana na nini
Na ile keki(Nilikata ya nini?)
Na mahari(Nililipa kwa nini?)
Na yule mshenga(Nilimtuma wa nini?)
We si uliapa tena ukala yamini
Naubembeleza upepo
Usizime kibatalii(Iye iye iye)
Kichwani mwangu hayupo
Moyoni niko shwari(Iye iye iye)
Ona hajaacha pengo mwambie, asiwaze
Huko aliko atulie, asiwaze
Kama amepoteza lengo mwambie, asiwaze
Huko aliko atulie, asiwaze
Wewe ambaye hujaolewa
Usifanye kama hutaki kuolewa hivi eeh
Alafu na wewe ambaye hujaoa
Sio kwa sababu ya nyimbo
Eti ukakata tamaa ya kuoa(Mmmh mmh)
Sijasema hivo aiseee
Asiwazee! Hata akinisema popote pale
Asiwazee! Na hata tukionana mahala popote pale(Asiwaze)
Bear, Peace! I live my life men
Kiri Records
Lets take over the game
Ecouter
A Propos de "Asiwaze"
Plus de Lyrics de STAMINA
Commentaires ( 0 )
Aucun commentaire pour l'instant
Vous aimeriez sûrement
Essayez l'application Mobile
A propos de AfrikaLyrics
Suivre Afrika Lyrics
© 2024, We Tell Africa Group Sarl