Paroles de Kiguu na Njia
Paroles de Kiguu na Njia Par MR BLUE
Never loose, yeah yeah yeah
Nimehustle miaka mingi
Eti mpaka leo bado niko kwenye mbio
Kwa kusaka shilingi
Eti mpaka leo sioni mafanikio
Nyumbani hakuna raha
Kila siku ni vilio
Watoto wanalia njaa aah
Kero kwenye masikio
Ila one day nitapata na mimi
Walopata wana nini
Na mimi nimekosa, nimekosa nini
Ila one day ye ye ye
Kama Mungu namuamini
Na mi najiamini
Sasa niko na nini?
Kiguu na njia oooh
Jua linatoka na kuzama nipo kwenye njia
Kushoto na kulia oooh
Ila Mungu yupo na nia na sitakata tamaa
Kiguu na njia oooh
Jua linatoka na kuzama nipo kwenye njia
Kushoto na kulia oooh
Ila Mungu yupo na nia na sitakata tamaa
Jua linawaka
Mwenzenu nimechoka
Mifuko imetoboka
Mi nasota ye ye yeee
Kama Mungu wangu yupo
Basi najua ipo hata nikipata mwisho
Labda kinikute kifo
Ila Mungu yupo na subiri nione mwisho
Lazima nichukue jiko
Ah hakuna jiko bila mshiko
Vyakula kwa vijiko
Madiko diko mpaka tunalamba mwiko
Ila one day nitapata ghetto kuu
Mmoja wa kuwa na mimi
Kuniamini kunidhamini
One day ye ye yeee
Kama Mungu namuamini
Na mi najiamini
Sasa kuna nini?
Jua linatoka na kuzama nipo kwenye njia
Kushoto na kulia oooh
Ila Mungu yupo na nia na sitakata tamaa
Kiguu na njia eiyee
Jua linatoka na kuzama nipo kwenye njia
Kushoto na kulia oooh
Ila Mungu yupo na nia na sitokata tamaa
Jua linawaka
Mwenzenu nimechoka
Mifuko imetoboka
Mi nasota ye ye yeee
Ecouter
A Propos de "Kiguu na Njia"
Plus de Lyrics de MR BLUE
Commentaires ( 0 )
Aucun commentaire pour l'instant
Vous aimeriez sûrement
Essayez l'application Mobile
A propos de AfrikaLyrics
Suivre Afrika Lyrics
© 2025, We Tell Africa Group Sarl