MOTRA THE FUTURE Hautaki cover image

Paroles de Hautaki

Paroles de Hautaki Par MOTRA THE FUTURE


Kimambo on the beat

Ndoto zako zilikuwa kuzaliwa ulaya
Umezaliwa nchi hautaki
Baba haumtaki na mama hautaki
Hta kaka na dada zako wote, huwataki
Maana wana maisha ambayo wewe hauyataki
Mmezungukwa na majirani ambao hauwataki
Ghafla unaanza kukua lili life hautaki
Unajikuta unapelekwa shule ile hautaki
Unapata marafiki wale wenye hautaki
Walimu na masomo ni wale hautaki
Ile shule hautaki na walimu hautaki
Inakupea division ambazo wewe hautaki
Unapata hasira ambazo wewe hautaki
Ukiwaza kujiajiri una gundua hautaki
Kisha unaajiriwa kazi ambayo hautaki
Nayo inakulipa mshahara ambao hautaki
Kazini napo mbali kutembea hautaki
Unajikuta unaenda kununua gari hautaki
Kila siku ni matengenezo na kupaki
Linakurudisha nyuma kulekule hautaki
Unajiskia upweke na wewe usingle hautaki
Na hio sura mbaya unapata mpenzi hautaki
Ukijua ni one time life time hautaki
Unaskia kashika mimba nan do kile hautaki
Unajikuta tu una familia hautaki
Wanaingilia kati wale ndugu hautaki
Wanakufungisha ndoa na yule demu hautaki
Mapenzi kedekede hatakama hautaki
Unatoa machozi na kulia hautaki
Damn
Kuishi life hautaki
Unaweza ukajiona bitch vile life inaku fuck
Ndo ile umezeeka na kustaafu hautaki
Unapata kiinua ngongo ambacho nacho hautaki
Unapata stress unaumwa magonjwa hautaki
Huna bima, unapelekwa hospital hautaki
Unaanza poteza tumaini na ndo kitu hautaki
Ghafla anakuja Israël na wewe kufa hautaki
Unajikuta unaokoka na ulikua hautaki
Unamrudia mungu nae mungu hakutaki
Sema anakusamamehe haana ashakuona waki
kwani amekupa uhai ulivyo fala hautaki
Familia wanakuhurumia wakiumia hautaki
Ndugu wanajikusanya wakuchangi hautaki
Faraja hautaki, mapenzi hautaki
Japo hela umepokea na ulisema hautaki
Mwanao kakua akajitegemee wewe hautaki
Wakati akikaa tu nyumbani napo hautaki
Kumbe mshenga alikuja aolewe hautaki
Eti unataka hela kubwa mahari ndogo hautaki
Mtoto hadi akalia na akilia hautaki
Unambembeleza anyamaze akicheka hautaki
Na kila anchotaka yeye akisema hautaki
Kubali una roho mbaya ama nayo hautaki
Hata nikiuliza ni kwanini kila kitu hautaki
We mwenywe hautaki kwanini hautaki
Tukikwambia umelogwa kusikia hautaki
Na hata maswali yangu unadai hautaki
Hautaki tu kuongea hujiskii hautaki
Nimekwambia kuwa mchawi nao uchawi hautaki
Basu mimi naondoka nikikaa si hautaki
Cha ajabu nakuaga hata hio bye hautaki

Hehe ouuh yee
Baba ako pon de ting
Am out

Ecouter

A Propos de "Hautaki"

Album : Hautaki (Single)
Année de Sortie : 2021
Ajouté par : Farida
Published : Jan 06 , 2022

Plus de Lyrics de MOTRA THE FUTURE

MOTRA THE FUTURE
MOTRA THE FUTURE
MOTRA THE FUTURE
MOTRA THE FUTURE

Commentaires ( 0 )

Aucun commentaire pour l'instant



A propos de AfrikaLyrics

Afrika Lyrics est la plus large collection de paroles de chansons et de traductions d’Afrique. Afrika Lyrics fournit les paroles des musiques de plus de 30 pays africains et des traductions de lyrics de plus de 10 langues africaines en français et en anglais.

Suivre Afrika Lyrics

© 2025, We Tell Africa Group Sarl